Mheshimiwa Spika;
Niko hapa leo
kutimiza matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 91
Ibara ndogo ya kwanza inayonitaka kulihutubia na kulifungua rasmi Bunge hili.
Naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afya njema, na
kutuwezesha kuwepo hapa siku ya leo.
Aidha nitumie fursa hii kuwakumbuka wenzetu
ambao, kwa namna na nafasi mbalimbali, walishiriki katika mchakato wa uchaguzi
huu na kwa bahati mbaya walipoteza maisha yao kabla ya mchakato haujakamilika.
Kwa hao wote waliotangulia mbele za haki ninamuomba Mwenyezi Mungu azirehemu
roho zao na awape pumziko la amani.
Nitumie nafasi hii kuwapa pole ndugu na
jamaa ambao ndugu zao walifariki na wengine kupata ulemavu wakati wa mchakato
wa uchaguzi huu. Kusoma hotuba kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...