Kituo kipya na cha kisasa kimefunguliwa huko Bagamoyo, eneo la Ukuni, Mkoa wa Kwani kikiwa na huduma nzuri, kuanzia malazi, chakula bora na usafi wa hali ya juu na kipo sehemu tulivu tayari kuwasaidia waathirika wa madawa ya kulevya na ulevi wa pombe kupindukia, ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha kwa njia ya ushauri nasaha na kuwarudisha katika hali timamu.
Kituo hiki cha aina yake kina wataalamu waliobobea kila idara.Pia kuna daktari wa afya.Kituo pia kinatoa mafunzo ya ujasiriamali na mafunzo ya kompyuta pindi mwathirika anaporejea katika hali ya utimamu.
Hali kadhalika kituo hiki pia huwatafutia waliopata nafuu wafadhiri ili waweze kupata mafunzo kwenye vyuo vya ufundi vya serikali vya VETA kama vile useremala, udereva, ufundi umeme, fundi wa magari na kadhalika.
Kwa mawasiliano piga simu namba 0714 119494/0676948829/0718512627
Email info@lifehope.or.tz website www.lifehope.or.tz
Lango kuu la Life and Hope Rehabilitation Centre (Bagamoyo Sober House).
Mandhari ya Life and Hope Rehabilitation Centre (Bagamoyo Sober House).
Sebule ya Life and Hope Rehabilitation Centre (Bagamoyo Sober House).
Sehemu ya malazi katika Life and Hope Rehabilitation Centre (Bagamoyo Sober House).
Kompyuta za kisasa kwa wataopitia Life and Hope Rehabilitation Centre (Bagamoyo Sober House).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...