Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru leo ameanza kazi na kuwataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kuwahi kazini kwa wakati na kufanya kazi kwa bidii. 
Profesa Mseru ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam baada ya kukutana na menejimenti ya hospitali hiyo ambayo inajumuisha Wakurugenzi 14. 
Mkurugenzi huyo amekutana na menejimenti hiyo majira ya saa 6:00 mchana katika ukumbi wa mikutano wa hospitali hiyo. 
Pia, amekutana na kamati tendaji ya hospitali , wakurugenzi, wakuu wa idara, mameneja wa majengo ikihusisha Sewahaji, Mwaisela, jengo la watoto na jengo la wazazi saa 8: 00 mchana. 
Pamoja na mambo mengine katika kikao hicho, wakurugenzi wameeleza mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo. 
Profesa Mseru ameteuliwa jana kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo baada ya Dk Hussein Kidanto kuhamishiwa wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma (MNH), Aminiel Aligaesha (kulia) na akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali hiyo Profesa Lawrence Mseru kwa kamati tendaji, wakurugenzi, wakuu wa idara, mameneja wa majengo ya Kibasila, Sewahaji, Mwaisela na Jengo la Watoto. 
 Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru (kulia) akizungumza na kamati tendaji, wakurugenzi, wakuu wa idara, mameneja wa majengo ya Kibasila, Sewahaji, Mwaisela na Jengo la Watoto.
Kamati Tendaji, wakurugenzi, wakuu wa idara, mameneja wa majengo ya Kibasila, Sewahaji, Mwaisela na Jengo la Watoto wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru 
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Hussein Kidanto (kushoto) akishukuru watumishi wa hospitali hiyo na kumtambulisha  Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Mseru (kulia) ambaye ameteuliwa jana na Rais John Pombe Joseph Magufuli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Naona manesi mmeinamisha vichwa chini tu. Tafadhali jamani inueni mioyo muwe na utu na maisha ya watu.

    ReplyDelete
  2. Aende tu si mtumishi bora

    ReplyDelete
  3. Prof mseru do your thing

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...