Kumekuwa na sheria na kanuni mbalimbali zinazoundwa, ingawa wakati mwingine hushindwa kutekelezeka kwa wakati. Ukifika katika hoteli ya Golden Tulip utakuta jinsi eneo hilo linavyozidi kujengwa na kuendelezwa kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu. Kujengwa kwa eneo hili lililokuwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi ni kinyume cha sheria ya Hifadhi ya Bahari. Tumeshuhudia maeneo mengi yakivunjwa kwa nyumba zao baada ya kubainika yamejengwa katika hifadhi ya bahari. Haijafahamikaa mara moja kama eneo hili limeruhusiwa kuendelezwa, ikiwa ni tofauti na jengo la Hoteli ya Golden Tulip
Sheria za Hifadhi ya bahari inasema ni marufuku kujenga nyumba mita 60 ilipokuwa bahari. Hali hii imeonekana kuwa tofauti baada ya kukuta hifadhi hii ikionekana kuanza kujengwa na kuanza kuzua maswali mengi kwa wadau wa maendeleo na Waanzania kwa ujumla wanaofuatilia mambo ya maliasili na utalii. Kibao hiki kinaonyesha jinsi eneo hilo lilivyotengwa kwa ajili ya kujenga jambo ambalo ni kinyume cha sheria za mita 60 za bahari.
Gari likipita katika barabara inayoelekea katika barabara ya Golden Tulip Hoteli, ambayo pia inaonekana eneo hilo lililowekwa mabati kwa ajili ya kuanza kulijenga kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu. na chini mkazi wa jiji la Dar es Salaam akipita katika eneo hilo, huku ikionekana ramani mbalimbali za ujenzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nimeshangaa na kujiuliza maswali mengi sana,hasa ikikumbukwa kuwa hata ujez]nzi wa Hotel iliyopo ya Golden Tulip ulikuwa na maswali mengi sana,Je ni nani aliyetoa kibali hapa?je matumizi ya ardhi yamebadilishwa?Nadhani ni mfululizo wa mashaka ya maamuzi ya watu wa Wizara ya Ardhi.
    Maeneo kama haya ingekuwa ni busara kuhifadhiwa kwa kujengwa viwanja vya michezo mbalimbali ambavyo havitakuwa na majengo ya kudumu!!

    ReplyDelete
  2. Nampongeze Mh. Kikwete kwa kukataa kuzindua ujenzi huu pamoja na kupewa shinikizo na wahusika siku za mwishoni. Maana jamaa walishatoa mwaliko kwa wafanyabiashara wote Dar kwenda kwenye uzinduzi wa ujenzi huo awamu ya pili (wenyewe wanauita phase 2) ambao ulitarajiwa kuzinduliwa na Mh. Kikwete lakini naona baadaye Mh. aliwashtukia hivyo hakutokea. Mh Magufuli funga mkanda, kaza mwendo kazi kubwa iko mbele haswa kurekebisha madudu za zamani kama haya. Hapa Kazi Tu! - Mdau Joe Bura dar

    ReplyDelete
  3. The mdudu, hao lazima watoke wasitake kutuhalibia nchi yetu na mafukwe yetu na waliohusika wote waburuzwe mahakamani na wafungwe pia ili iwe fundisho kwa washenzi kama hao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...