Mkutano wa kila mwaka wa Kuwezeka umeme Afrika: Kongamano la Uwekezaji
la Tanzania litafanyika Hyatt Regency Dar es Saalam, Hoteli ya Kilimanjaro
kuanzia 3-4 Desemba 2015
Mkutano ule utalenga siku za usoni za sekta ya kawi ya Tanzania
kufuatia uchaguzi wa hivi majuzi, kutambua nafasi za uwekezaji na kubuni
maushurikiano muhimu kati ya wahusika kutoka sekta ya kibinafsi na ya
umma.
Dhibitisho za hivi karibuni za January Makamba, Mbunge wa Bumbuli,
Tanzania, waakilishi kutoka Kitengo cha Rais cha Utekelezaji (PDB), Wizara ya
Kawi, Madini na Kampuni ya Usambazaji wa Gesi (GASCO) zinaashiria juhudi
zinazoendelea katika sekta ya umma kuharakisha ufikiaji wa kawi nchini Tanzania
kama hatua muhimu katika ukuzaji wa uchumi.
Hadi sasa, kampuni 37 za kipekee kutoka sekta ya kibinafsi
zimedhibitishwa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Tanzania,
Standard Chartered Bank, Mitsubishi Corporation, CitiBank Tanzania, BVI
Consulting, Liquefied NG Tanzania, Statoil na Sunfunder.
Yale mazugumzo yatalenga mijadala kama vile kujitolea kwa Tanzania kwa
mageuzi ya sekta ya kawi, ukuaji wa kitengo hicho pamoja na ukuzaji gesi,
mbinu za Tanzania za ununuzi katika sekta za kampuni za umma na umuhimu wa
umeme kwa kilimo katika viwanda husika vya kuzalisha kawi.
Kufuata ufadhili wa hivi karibuni wa dola za Marekani milioni $5
kutoka IFC kuwezesha Tanzania kuchunguza uwezo wa mitambo ya kawi iliyo ya
nguvu za chini, mpangilio ule utachunguza pia njia mbalimbali za kupeana
kupasisha kawi hadi nchini Tanzania na nafasi za kawi ya zitokanazo na jua,
upepo, joto na maji, kama maendeleo ya ukuzaji wa kawi.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...