Bondia Hamisi Mwakinyo kushoto akitunishiana misuli na Meshach Mwankemwa baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na  Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC  katikati ni promomota kutoka katika kampuni ya Golden boy Afrika Shomari Kimbau Picha na SUPER D BOXING NESW.

Promota Shomari Kimbau akiwainua mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


 Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa akiwakumbusha baadhi ya sheria zitakazo tumika katika mchezo wa ngumi utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Dar es salaam.

NA Mwandishi Wetu
MABONDIA Meshack Mwankemwa na Hamisi Mwakinyo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa kg 66 unaotambuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchi mkanda uho uliokuwa umeachwa wazi na bondia Selemani Zogo kwa kuto utetea kwa wakati sasa utapiganiwa na mabondia hawo kesho

akizungumza wakati wa upimaji wa uzito promota wa mpambano uho Shomari Kimbau amesema mkanda uho utapiganiwa na mabondia hawo ili apatikane bingwa mpya wa uzito wa kg 66

mpambano uho utasimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini chini ya rais wake Chauremba Palasa aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo pia kutakuwa na ngumi za utangulizi za mabondia mbalimbali

Said Mayanga atamenyana na Gido Selemani wakati Mohamed Amir atapambana na Hemed Hemed

na mpambano mwingine wa kusisimua utakuwa ni wa akina mama ambapo bondia mnaschachali Asha Nzowa 'Asha Ngedere' atapambana na Joyce Awino ambambao ambao unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wanawake wa mchezo wa masumbwi  


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...