Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (Pichani) amesema wananchi ambao hawajaweza kupata haki zao katika mahakama za mwanzo wanaweza kutumia kamati ya maadili.

Makonda ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Makonda amesema kuwa watu wengine wanakosa haki katika mahakama na hawajui wanaweza kupata haki sehemu gani kutokana na mwenendo wa kesi ilivyoendeshwa.

Makonda amesema kamati hiyo inawajibu wa kuangalia mwenendo wa maadili ya hakimu na ikibanika kamati inaweza kuchukua hatua.

Amesema kuna baadhi ya wananchi wanapewa hukumu za kesi lakini mwenendo wa kesi haujui na mwisho wa siku anakosa haki kutokana na baadhi ya watu kutumia mahakama vibaya.
Makonda amesema sharia ya Usimamizi wa Mahakama  Na.4 ya mwaka 2011 sehemu 51(1) kutakuwa na kamati ya mahakama ya wilaya  ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya.

 Aidha amesema wengine wanaounda kamati hiyo ni Hakimu Mkazi wa Wilaya au msimamizi wa Wilaya ,Katibu wa Tawala wa Wilaya  (DAS) ambaye anakuwa Katibu wa Kamati hiyo,Kiongozi wa dini mmoja ambaye atateuliwa na Mkuu wa Wilaya ,mtu mashuhuri wa wilaya ambaye ni mwadilifu.
Hata hivyo amesema katika kamati hiyo maafisa wawili watateuliwa na Jaji  anayesimamia .
Kamati hiyo itawajibika kupokea na kuchunguza malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi kuhusu mahakama na kuwasilisha ripoti kwa tume.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huyu mkuu anakurupuka kama bata mzinga. Does he knows the meaning of Republic of Tanzania? To be Republic the country has to have Executive, Legislative and Judicial branch. Civic kama umesahau.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...