Mnamo tarehe 22/10/2015 kijana mmoja wa Kiswedish alivamia shule ya Krona iliyopo mji wa Trollhatan uliopo jirani na mji wa Goteborg ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Sweden.
Kjjana huyo alivamia shule hiyo akiwa amevalia mavazi ya Halloween na kuanza kuchoma visu watoto . Alifanikiwa kuchoma visu walimu wawili na watoto wawili na maaaskari wawili kabla ya polisi kumpiga risasi na na kumuua dunia hapo hapo. Watu aliowajeruhi walikimbizwa hospital ambapo mwalimu mmoja na mwanafunzi mmoja walifariki dunia na wengine wailipona.
Baada ya kumpekua, Polisi walikuta barua yenye maelezo na sababau ya huyo muuaji kuamua kufanya hivyo. Aliandika kuwa nimeamua kufanya mauaji haya kwa sababu sikubaliana na serikali yangu kwa sasa kukubali wimbi la wahamiajai kuongezeka. Hali kwa sasa imekua ni tete ambapo karibu kila wiki kwa nyumba wanayoishi wahamiaji imekua ikichomwa moto au kambi waliyokua wamehifadhiwa wakimbizi toka sirya.
Tarehe 13/10/2015 ndio yalikua mazishi ya kijana huyo wa Kiafrika aliyeitwa Ahmed Hassan aliyefariki katika mauaji hayo ya kibaguzi na kuzikwa na maelfu ya watu toka ndani na nje ya Sweden.
Baada ya mazishi na huduma za chakula cha mchana kilichoandaliwa na Tanzanian Restaurant kwa wageni maalumu tu ambao walifikia 1000. Mgahawa huu wa Chakula cha Kiafrika unaendeshwa na Executive Chef Issa Kipande, ambaye pia ni blogger nguli na mwanachama hai wa Tanzania Bloggers Network (TBN).
Chef Issa akiwa na Gustav Fridolin waziri wa elimu wa Sweden wakati wa chakula cha mchana amvcho kilihudumiwa na mgahawa wake anaoendesha wa Tanzanian restaurant kwa wageni maalumu tu ambao walifika 1000.
Akiwa na Paul Akerlund Meya wa jiji la Trollhattan
CHef Issa akiwa na mmoja wa watu mashuhuri waliofika kutoa rambi rambi na kulaani kitendo hicho ni pamoja na Bw. Mohamed Adulahi Mohamedi almaarufu kama "Farmajo' ambaye alikua waziri mkuu wa Somalia kati ya mwaka 2010 na 2011,
Chef Issa akiwa na Monica Hanson, Meya msaidizi wa jiji la Trollhattan
Eneo la tukio mnamo tarehe 22/10/2015 ambapo kijana mmoja wa Kiswedish alivamia shule hii ya Krona iliyopo mji wa Trollhatan uliopo jirani na mji wa Goteborg ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Sweden.
Sehemu ya umati wa waombolezaji tarehe 13/10/2015 kwenye mazishi ya kijana huyo wa Kiafrika aliyeitwa Ahmed Hassan aliyefariki katika mauaji hayo ya kibaguzi na kuzikwa na maelfu ya watu toka ndani na nje ya Sweden.
Matukio kama haya yanatukumbusha kitu kimoja: Nyumbani ni nyumbani. Huko "majuu" hata mkipata fedha nyingi na kupewa uraia si kwenu na hamna raha na amani kama mtu aliyeko nyumbani. Nyumbani kwenu ni Tz. Msilazimishe nchi za watu kuwa nyumbani kwenu. Mimi nikitembea tz sina wasi wasi ninyi mnaangalia kushoto na kulia sababu kuna wengi hawapendi ninyi kuwa huko. Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu na ipumzike kwa amani. Amen
ReplyDeleteINAKUAJE BINADAMU UMCHUKIE BINADAMU MWENZIO BILA YA SABABU
ReplyDeleteEndeleza kazi nzuri Chef Issa,unatuweka kwenye ramani katika sekta ya huduma za hoteli na mikahawa.
ReplyDeleteAma kweli uelewa huu mdogo. Endelea kujisikia nyimbani hapo ulipo. Walio nchi za watu nao wafurahie uraia na pesa nyingi. Mungu amlaze pema huyu tuliyempoteza bila sababu ya msingi.
ReplyDelete