Mrembo anayeshikilia taji la Urembo la Taifa (Miss Tanzania 2014/15) Lilian Deus Kamazima anatarajia kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. Said Meck Sadick  ikiwa ni ishara ya kumtakia kila la kheri katika mashindano ya urembo ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika Jijini Sanya, nchini China,  tarehe 19 Desemba 2015.

Mrembo huyo ataondoka nchini Ijumaa ya tarehe 20 Novemba 2015 na ataungana na warembo wengine kutoka nchi zaidi ya 120 duniani na watapiga kambi ya mwezi mmoja katika Hotel ya Beauty Crown, Sanya nchini China.

Lilian amekuwa katika maandalizi ya kutosha tangu achukue Taji hilo mwezi Oktoba 2014.

Pamoja na mambo mengine ameshiriki  Onyesho la Mavazi la nchi za Afrika ya Mashariki lililoandaliwa na Kampuni ya Arapapa Fashion ya mjini Kampala Uganda mwezi Novemba 2014 pia ameshiriki katika shughuli mbalimbali za Jamii katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Dar es salaam.

Kama Balozi wa Hospital ya CCBRT Miss Tanzania Lilian Kamazima ataondoka na ujumbe wa kupiga vita na kupambana na matatizo ya wasichana na akina mama ya Fistula.Mrembo huyo anatarajia kurejea nchini tarehe 20 Desemba, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...