Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla amekabibidhi vifaa vya michezo ikiwemo jezi, mipira,nyavu za magoli na vikombe kwa ajili ya timu ya wafungwa na askari gereza la Karanga Moshi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa hivi karibuni baada ya kufanya ziara gerezani hapo na kupokea maombi.
Katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni tatu na nusu aliwakumbusha wafungwa na mahabusu kuwa michezo hujenga umoja, michezo ni burudani, michezo ni kwa afya na zaidi kwa wenye vipaji michezo itumike kulinda vipaji vyao na siku wakitoka waviendeleze vipaji.
Vifaa alivyokabidhi ni pamoja na nyavu za magoli, vikombe 2 vya kushindaniwa,jezi kwa timu 5 za wafungwa na mahabusu, mipira 10 kwa ajili ya wafungwa na mahabusu, jezi moja na mpira mmoja kwa ajili ya timu ya netball ya wafungwa wanawake na jezi moja , mipira 3 na nyavu za magoili kwa ajili ya timu ya askari magereza.
Uongozi wa gereza, wafungwa na mahabusu wamemshukuru sana mkuu wa mkoa kwa msaada huo na wamemuhaidi kumuuenzi na kila mwaka watakuwa na ligi itakayoitwa Makalla Cup na wamewataka viongozi na wadau wengine kite nchini kuiga mfano. alioonyesha mkuu wa mkoa wa kilimanjaro
Sehemu ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Amos Makalla kwa Gereza la Karanga Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mh. Amos Makalla akipiga mpira kuashiria kuendeleza michezo Gerezani hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...