Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hii issue ina misingi ya sifa na kujionyesha, sidhani magufuli anapenda tabia kama hizi, rais alikwenda fadha akakuta kuna watu wengi hawapo ofisini kama rais hakuchukua uwamuzi wa kuwafunga ama kuwafukuza kazi, muhimbili hakuwafukuza kazi watumishi hata baada ya kukuta madudu kule. DC umepoteza 2 hrs pesa za walipa kodi kusubiri hao jamaa kwanini hukuanza kazi mara moja sasa unaigarimu serikali sku nyingine bila ya msingi wowote. Zaidi sana sijui kuwaweka hawa jamaa ndani kimeangaliwa kisheria? Please, post this comment.

    ReplyDelete
  2. Tz hususani karibu wananchi wengi wamekaa kwa muda mrefu sana tokea miaka ya 1980 hadi sasa bila ya kuzingatia sheria kutokana na baadhi ya viongozi wanaopewa madaraka kwa nia njema kuharibu kwa kutowajali wananchi kiasi imefikia kuwa kila mtu shauri lake. Baadhi ya viongozi hao kwa kutumia madaraka waliyopewa ndiyo chanzo kikubwa cha ukiukwaji uliyokithili hivi sasa. Baadhi yao wakishiriki Rushwa, kutokuwa waaminifu, dharau, pia wamesababisha kuzolota kwa mihimili ya usalama wa raia kama vile polisi, mahakama, ubaguzi wa elimu, kutowajali wanyonge na mambo mengine ya kuwanyima wananchi haki yao. Kizazi kilichokuwepo miaka ya 80 kimezaa kizazi ambacho wengi wamekosa uadilifu na weredi. Hivi sasa watumishi na raia wengi wamekosa weledi au nidhamu ya kuheshimu sheria za nchi, kutopenda kujituma, uvivu, kukosa uaminifu n.k.. Kwa hivyo sehemu kubwa ya kizazi hiki cha leo kimekosa maadili. Kwa vyovyote vile tunapongeza sana hoja ya "Hapa Kazi Tu," na ili kasi hii iweze kwenda vizuri kuna haja ya kuwa na mpango mkakati wa kuwaelimisha wananchi sheria za msingi za kuwalinda ili wasije wananchi wengi wakapata madhara ya kuvunja sheria na kuadhibiwa bila ya kuelewa kutokana na umbumbumbu wao wa kuzijua sheria. Pengine kuna haja kila mkuu wa wilaya au Mkoa kuandaa mikakati ya kuelemisha wananchi nchi nzima li wafahamu wajibu wao kisheria ili utekelezaji wa "Hapa Kazi Tu" upokelewe na uendelezwe bila ya malalamiko wala manung'uniko. Tanzania ni nchi iliyojaaliwa na tumejaaliwa kumpata kiongozi huyu mchapakazi na muadilifu. Tumuunge mkono kwa nguvu zetu zote!!

    ReplyDelete
  3. uliyokithili hivi sasa. Baadhi yao wakishiriki Rushwa, kutokuwa waaminifu, dharau, pia wamesababisha kuzolota kwa mihimili ya usalama wa raia kama vile polisi, mahakama, ubaguzi wa elimu, kutowajali wanyonge na mambo mengine ya kuwanyima wananchi haki yao. Kizazi kilichokuwepo miaka ya 80 kimezaa kizazi ambacho wengi wamekosa uadilifu na weredi. Hivi sasa watumishi na raia wengi wamekosa weledi au nidhamu ya kuheshimu sheria za nchi, kutopenda kujituma, uvivu, kukosa uaminifu n.k.. Kwa hivyo sehemu kubwa ya kizazi hiki cha leo kimekosa maadili. Kwa vyovyote vile tunapongeza sana hoja ya "Hapa Kazi Tu," na ili kasi hii iweze kwenda vizuri kuna haja ya kuwa na mpango mkakati wa kuwaelimisha wananchi sheria za msingi za kuwalinda ili wasije wananchi wengi wakapata madhara ya kuvunja sheria na kuadhibiwa bila ya kuelewa kutokana na umbumbumbu wao wa kuzijua sheria. Pengine kuna haja kila mkuu wa wilaya au Mkoa kuandaa mikakati ya kuelemisha wananchi nchi nzima li wafahamu wajibu wao kisheria ili utekelezaji wa "Hapa Kazi Tu" upokelewe na uendelezwe bila ya malalamiko wala manung'uniko. Tanzania ni nchi iliyojaaliwa na tumejaaliwa kumpata kiongozi huyu mchapakazi na muadilifu. Tumuunge mkono kwa nguvu zetu zote!!

    ReplyDelete
  4. HAPA KAZI TU HAKIKA NIDHAMU HAIZINGATIWI SIKU HIZI. HONGERA SANA MKUU WA WILAYA

    ReplyDelete
  5. MKUU KUNA KIWANJA TUMEDHULUMIWA NA WENYE PESA NA BABA AMEFARIKI TAYARI TUNAOMBA MSAADA WAKO. BABA AMEFATILIA SANA MPAKA KUPELEKEA KIFO CHAKE KWA PRESHA. KIPO MAENEO YA MWENGE NATAFUTA NAMBA YAKO PLSSSSSS

    ReplyDelete
  6. The mdudu, mdau wa kwanza hapo juu tulia dawa ikuingiie watu kama nyie ndio msioitakia Tanzania yetu isonge mbele sasa mbona povu chafu linakutoka? mimi nahisi wewe ndio mmoja wapo kati ya hao waliotupwa lupango kwa taarifa yako ukitaka kuondokana na #hapakazitu ni kupiga kazi kisawasawa muda wa kulipwa pesa huku hatuoni ulifanyaro haupo tena pongezi kwako MAKONDA wakondeshe kweli hao wazembe

    ReplyDelete

  7. Kutokea hapo nikaanza na process umpya, lakini mpaka leo bado napigwa chenga. Nimetumia watu wa kila aina lakini sijafanikiwa ukilalamika kwa watu wanakucheka kwanini unataka kufuata sharia wewe jenga tu. Mimi naishi nje ya nchi, kila nikija nyumbani likizo yangu huwa inaishia Ardhi! Yaani maudhi matupu.

    Lakini pia na kusumbuliwa kote huku, sidhani kama Mkuu wa wilaya amewatendea haki hawa watu. Naona amejichukulia sharia mikononi na kuingilia kazi ya police. Kuchelewa kufika kazini siyo kosa la jinai, yeye ambacho angefanya ni kuwaamuru kurudi kazini na waandike barua ya kujielezea kwanini wamechalewa na kuwaandikia warning. Sidhani kama Rais JPM anamaanisha kwamba utendaju wa kazi ufanywe kwa kuwaweka wafanyakazi wazembe rumande. Nafikiri Mkuu wa wilaya amemuelewa vibaya. Haya ni maoni yangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...