Nalimi Mayunga , mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars
Afrika, ameondoka nchini Jana kuelekea nchini Marekani kwa lengo la
kupata mafunzo na kurekodi nyimbo yake
Nalimi ameondoka usiku usiku wa kuamkia leo kwenda kufanya kazi na
nguli wa mzuki wa R&B nchini Marekani Bwana Akon ambapo anatarajiwa
kukaa muda wa wiki moja kisha kurejea nyumbani tarehe 24 Novemba.
Akiongea wakati halfa ya kumuaga, Afisa habari mwandamizi wa Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA), Aristide Kwizera alisema” Tunajisikia furaha
kuona vijana wa kitanzania wakitangaza sanaa na nchi yetu duaniani
kupitia muziki. Napenda kumpongeza sana mayunga kwa kupata ushindi
ambao umempatia nafasi hii nono na kumwomba atumie vyema fursa hii.
Sisi kama wadau wakuu wa sanaa nchini tunawapongeza sana Airtel kwa
kuanzisha program zenye lengo la kukuza sanaa na muziki wa nchini kama
hii ya Airtel Trace Music Stars na nyingine nyingi.
Naye mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi
Mayunga alisema” ile siku niliyokuwa naisibiria kwa hama leo imefika
na nimejipanga kuondoka kwenda kujifunza mengi na ya msingi katika
maisha yangu ya muziki . Naamini safari hii itakuwa ni ya mafanikio
makubwa na mwanzo wa hatua yangu ya mafanikia katika tasinia ya muziki
Napenda kuwaambia watanzania wajiandae kusikia kibao na video kali
ntakayoifanya na Akon kwani nimejiandaa vya kutosha kuhakikisha
nashirikiana nae vyema ili tunatoa nyimbo kali itakayowapa burdani
wapenzi wa muziki pande zote duniani", aliongeza Mayunga
Kwa upande wake Aliyekuwa jaji katika shindano la Airtel Trace Music
Stars Tanzania na Mwalimu wa Muziki Tony Joet alisema” Mayunga
amekuwa akifanya mazoezi kujiandaa kwa deli hii toka alipotangazwa
mshindi wa Airtel Trace Afrika.
"Nina imani naye kwani ameonyesha uwezo
mkubwa na nidhamu ya hali ya juu na naamini atafika mbali na namtakia
kila laheri katika safari yake”
Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane
Matinde alisema” mipango yote ya safari imekamilika na mayunga atakuwa
marekani kwa muda wa wiki moja, tunaamini mayunga atakaporejea atakuwa
tofauti kabisa na alivyokwenda na ndio hasa lengo letu sisi Airtel,
kuwawezesha na kuwainua vijana kubadilisha maisha na kufikia malengo
yao.
Shindano la muzuki la Airtel Trace Music stars lilizinduliwa octoba
2014 na huu ndio msimu wa kwanza wa shindano hili ambalo limewapatia
vijana watanzania na waafrika nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na
kupata fulsa mbalimbali za muziki.
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiongea na waandishi (hawapo pichani) wakati wa tukio la kumuaga kwa ajili ya kwenda kurekodi video ya mziki na kupata mafunzo toka kwa mwanamuziki wa kimataifa Akon nchini Marekani. hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Airtel Morocco jijini Dar Es Salaam. Pichani katikati ni Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde, akifatiwa na Mwalimu wa sauti Tony Joet.
Afisa uhusiano na mwandamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristed Kwizera (kushoto) akimuaga mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi kwa ajili ya kwenda kurekodi mziki na kupata mafunzo toka kwa mwanamuziki wa kimataifa Akon nchini Marekani katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Airtel Morocco jijini Dar Es Salaam. Anayeshuhudia (katikati),ni Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania jane matinde .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...