Msimu huu tutauliza iwapo habari zinazoangaziwa na mashirika ya habari zinawadhalilisha wanawake au la, tujadili pia shinikizo za kutakiwa kuwa ‘msichana mzuri’, pamoja na kutoa orodha ya kila mwaka ya ‘Wanawake 100’ huu ukiwa ndio mwaka wa tatu kufanya hivyo.
Msimu wa BBC wa Wanawake 100 utarejea mwezi huu, ukiangazia maisha ya wanawake maeneo mbalimbali duniani. Mradi wa Wanawake 100 ulizinduliwa 2013 na kuanzisha ahadi ya BBC ya kuwakilisha wanawake vyema kwenye habari zake kimataifa. Sasa katika mwaka wake wa tatu, msimu huu wa 2015 utajumuisha wiki mbili za mijadala, vipindi, makala maalum na uanahabari, na kifuchua wanawake 100 waliowatia motisha wanawake wengine mwaka huu.
Kwa wiki mbili kuanzia tarehe 18 Novemba, msimu wa Wanawake 100 utahusisha kutangazwa kwa makala maalum, vipindi na mijadala katika BBC World Service, bbc.com na idhaa za lugha 29 za BBC World Service na hata Network News
Fiona Crack, Mhariri wa msimu wa Wanawake 100 amesema: “Tunajivunia Wanawake 100 - kwa miaka miwili iliyopita tumetenga wakati mwingi na nafasi kwenye majukwaa na idhaa zetu kuwasilisha habari na kuangazia masuala yanayowaathiri wanawake popote walipo ulimwengu- kama vile watazamaji wetu walivyosema wangelitaka. Mwaka huu tutazindua akaunti za Facebook na Instagram na kuuliza iwapo wanawake wanakubali au kukataa shinikizo na matarajio ya kuwataka wawe ‘mwanamke mwema’ ama kwa watazamaji wadogo ‘msichana mzuri’ – tunataka kusikiliza maoni yao kuhusu sura ya uongozi na uhusiano.’
BBC Swahili itaanza msimu huu kwa kuangazia Wanawake Uongozini. Kipindi cha Amka na BBC cha Kesho asubuhi kitashirikisha mahojiano na mbunge mwanamke ambaye anajiunga na bunge la nchi hiyo la kumi na moja lilofunguliwa Jumanne, 17 Novemba. Kipindi cha jioni cha Dira ya Dunia kutakuwa na Mjadala mfupi utakaowashirikisha kina mama wabunge kutoka Kenya, Rwanda na Tanzania. Katika vipindi vitakavyofuata tutaangazia upatikanaji wa vyoo kwa wanawake na wanawake katika uuguzi na hata mada nyingine za kuvutia katika msimu huu.
Msimu wa Wanawake 100 hupangwa na kuandaliwa na idhaa za lugha 29 za BBC. Wasikilizaji wanaweza kujiunga na mjadala kwenye Twitter wakitumia #100women
BBC huvutia wasikilizaji, watazamaji na wasomaji milioni 283 kwa huduma zake za kimataifa za habari ikiwemo BBC World Service, runinga ya BBC World News na bbc.com/news.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...