Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam,Rais Mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hasani Mwinyi amewataka watanzania kuchangamkia fursa za masomo ya taaluma mbalimbali nanayotolewa na Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa mahafali ya tatu ya chuo hicho kwa upande wa Tanzania jana ambapo wahitimu walitunikiwa shahada ,stashahada na vyeti vya kufuzu fani mbalimbali alisema chuo hicho kinatoa elimu bora kwenye fani mbalimbali na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa za kujiendeleza ili wapate maarifa ya kuwawezesha kupambana katika soko la ajira ikiwemo kupata maarifa ya kuwawezesha kujiajiri kutokana na elimu watakayokuwa wameipata.
Alipongeza wawekezaji kwenye sekta ya elimu na kuiomba serikali kushirikiana nao li nchi iweze kupata wataalamu wa kutosha “Napongeza kwa uwekezaji huu na tunaomba serikali izidi kuunga mkono wawekezaji katika sekta ya elimu ili Taifa liweze kupata wataalamu wa kutosha.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mohamed Ndaula alisema kuwa chuo kimejipanga kuendelea kutoa elimu bora kuanzia kwenye miundombinu na walimu waliobobea katika fani mbalimbali na uzoefu mkubwa wa kufundisha vyuo vikuu sehemu mbalimbali duniani.
Pia alisema kuwa Chuo hicho kimefanikiwa kupata leseni ya kujiendesha nchini badala ya kuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu Cha Kampala kilichopo nchini Uganda.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi akiongozana na wahadhiri wa Chuo Kikuu hicho wakielekea kwenye uwanja wa hafla ya mahafali yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi (watatu kutoka kulia) na viongozi wa chuo hicho wakiwa wamesimama wakati unaimbwa wimbo wa Taifa kabla ya kuanza hafla ya mahafali ya 3 yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana jana ambapo wahitimu walitunukiwa shahada,stashahada na vyeti katika fani mbalimbali.
Sehemu wa wanafunzi waliohitimu chuoni hapo jana.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Kampala Internatinal cha Dar es Salaam Profesa Mohamed Ndaula akitoa hotuba wakati wa mahafali 3 yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana jana ambapo wahitimu walitunukiwa shahada,stashahada na vyeti katika fani mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...