Baadhi ya Wagonja walifikishwa Hospitali hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu  baada ya kupata maradhi ya matumbo ya kuharisha (kipindupindu).
 Mwandishi wa Habari Rahma Suleiman akichukua maelezo kwa Mgonjwa aliyefika katika kituo hicho mara baada ya kupata hujambo.
 Naibu Waziri wa Afya  Mahmoudu Thabiti Kombo akionyesha ramani ya maeneo yanayoathiriwa zaidi na ugonjwa wa maradhi ya matumbo.
Naibu Waziri wa  Afya  Mahmoudu Thabiti  Kombo akipata maelezo kwa Dkt. Dhamana  Fadhili Ramadhan  wakati alipotembelea wagonjwa wa maradhi ya kuharisha (kipindupindu) katika kituo cha Afya kiliopo Sheha ya Karakana. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. angalau na nyie sasa mnatembea kujionea hali halisi, mlizoea kuambiwa tu, tinga tinga linakuja, fanyeni kazi jamani acheni mazoea ya ubosi wa paper work tu

    ReplyDelete
  2. Magufuli embu pita na hapo.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana mlioathirika na maradhi haya, Mwenyeez Mungu atawaafu na kuwajaaliya shifaa. Lakini jamani hicho kitanda cha mayowe (cha kamba) hivi mtu katika hali yake ya uzima keshawahi kukilalia bila ya mkeka au godoro? Au kwa vile hao ni wagonjwa na kwa pengine ndio weshakatiwa tamaa, inatilisha imani kwa kweli, kheri ukagaragara sakafuni kuliko hizo kamba zinavyoumiza. Sina hakika kama wamefanyiwa hivyo kwa maana maalumu, nisijekuwa nalaumu nikakosea. Poleni sana maradhi kuingia rakhisi lakini kutoka yataka stahamala. Uguweni pole jamani.

    ReplyDelete
  4. Mahamoudu thabit kombo nI naibu waziri wa afya serikali ipi??
    Nadhani tuwe makini Mh Rais Magufuli hajatangaza hata Waziri Mkuu na Baraza lake.
    Na kama ni wa zanzibar basi tufahamu serikali ya zanzibar haina mawaziri kwa sasa.

    Kama ndugu kombo kashinda uwakilishi basi apewe heshima ya uwakilishi na sio u naibu waziri.

    ReplyDelete
  5. WAKUU WOTE Waende site sio kukaa ofisini. Rais hawezi tembelea maeneo yote na kwa kuwa watendaji wapo wafanye hiyo kazi vinginevyo mtamchosha rais wetu.ila pia Rais ashtukize Amana na Mwananyamala hospitsls

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...