NA BASHIR YAKUB -
Unapomdai mtu kupitia mahakanma na hukumu ikatolewa kuwa ni kweli unamdai na anastahili kukulipa basi mtu huyo hustahili kulipa. Lakini mara kadhaa hutokea mtu kusema sina hela ya kulipa au vinginevyo ilimradi tu asilipe deni.
Lakini pia madai hapa si lazima iwe hela tu inayotokana na kukopeshana. Yapo pia madai ambayo hutokana na mtu kushinda kesi. Kwa mfano mwanamke alifungua kesi dhidi ya mme wake akitaka matunzo yake na ya mtoto/watoto. Au shauri limekwisha na mtu aliyeshindwa ametakiwa na mahakama kulipa gharama. Au malipo ya fidia na mengineyo yote ambayo huamuliwa na mahakama kuwa yalipwe. Haya yote unaweza kuyafanya yalipwe kwa kukamata mshahara wa mhusika kwa njia za kisheria .
Hatua hii imeelezwa katika amri ya 21 ya kanuni ya 47 ya sura ya 33 ya sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai.
1.HATUA YA KUKAMATA MSHAHARA WA MTUMISHI.
Mahakama inapotoa hukumu ikimtaka mtu fulani kutekeleza jambo fulani au kulipa kiasi fulani kwa mtu fulani amri hiyo hutakiwa kutekelezwa kwa hiari na si vinginevyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...