Mbunge mteule wa Jimbo la Mtama, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape akisaini mkataba wa kupata vifaa vya huduma za afya mbele ya Mwambata wa Siasa wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Mis Song Rui katika ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China.

Mbunge Mteule wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye ameanza kazi ya kuwatumikia wakazi wa jimbo hilo baada ya kusaini mkataba maalum na Ubalozi wa China nchini wa kusaidia vifaa vya huduma ya Afya kwa jimbo la Mtama.

 Ikumbukwe katika kampeni zake Nape aliahidi kulifanya jimbo kuwa la mfano kwa kuboresha huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi Nape alisema " Wakati nimeamua kugombea ubunge nilisema nataka kuwafanyia kazi watu wa Mtama nataka niwe mbunge wa mfano na niliwaahidi nitatatua kero zao mbali mbali na leo nimeanza kwa upande wa huduma za afya ambapo vituo na zahanati kadhaa vitapata vifaa vya matibabu alivitaja baadhi ya vituo ni Mtama, Nyangamala, Chiponda, Namupa, Chiuta,Luo, Nyengedi,Kiwalala na kwengineko."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tuache omba omba kwenye Balozi. Wanatucheka na kutudharau.Ni njia yao yakununua influnce kwa wanasiasa wetu kwa kusingizia kusaidia majimbo yao. Nimeona wabunge wengi wateule wakikimbia kuwahi foleni kwenye Balozi hapa mjini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...