Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja juzi jumamosi ya 7 November 2015 walifanikiwa tena kwa mara nyingine kukonga nyoyo za washabiki mjini Bremen Ujerumani katika onyesho la kusherekea miaka 10 ya Pan African Organisation  lililofanyika katika ukumbi wa Bugerhaus Weserterasse.
Kikosi kazi kazi hiko cha FFU-ughaibuni kikiwa na madansa wao wawili Jessicha Ouyah na Sara Fina waliweza kulimudu jukwaa na kuwadatisha akili washabiki. Ngoma Africa band ipo katika medani ya muziki kwa takribani miaka 22 sasa na kuweka rekodi ya bendi pekee ya Kiafrika barani Ulaya inayodumu muda mrefu na kuwanasa washabiki wa kimataifa. wasikilize at www.ngoma-africa.com
Kamanda Ras Makunja akiongoza gwaride jijini Bremen
Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni wakipiga kwata Bremen
Ukumbi wa Bugerhaus Weserterasse ukiwashwa moto na FFU Ughaibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ngoma Afrika band aka ffu aka viumbe wa ajabu Anunnaki aliens aka watoto wa mbwa #Hapa Kazi TU

    ReplyDelete
  2. FFU MBELE KWA MBELE KASI HILE HILE KAMANDA

    ReplyDelete
  3. Mkuu kamanda baona kikosi kinathibiti ulinzi katika himaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...