SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeanza
kampeni ijulikanayo kama NSSF
Kwanza ambayo itafanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, Kampeni hiyo
imeanza kwa kuwafikia wakulima kwenye vijiji vyao na Mashamba yao Mkoani Mbeya ili kuweza kuwapa elimu juu ya
hifadhi ya jamii na faida zake.
Kampeni hiyo imeanzia kwenye Kijiji cha Iyumpi wilayani
Mbozi ambako wakulima wa Kahawa zaidi ya 44 wamejiunga na NSSF. Pia Kampeni
hiyo inatarajia kwenda Wilayani Ileje, Vijiji vya Mloo na Igamba.
NSSF inaendelea kuwasihi Wakazi wa Mbeya na Vitongoji vyake
waendelee kujiunga na NSSF ili waweze kujipatia Mafao bora yakiwemo Bima ya
Matibabu bure kwa Mwanachama na familia yake.
Wakazi wa Kijiji cha Itumpi wilaya ya Mbozi wakiwa wamekusanyika ili kusikiliza elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima kupitia Mpango maalumu wa Wakulima Scheme kwenye kampeni inayoendeshwa na NSSF ijulikanayo kama NSSF Kwanza.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Salim Kimaro akitoa elimu kwa wakazi wa kijiji cha Itumpi Wilaya ya Mbozi juu ya mpango wa Wakulima Scheme .
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...