Wapili kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa kijamii wa PSPF Adam Mayingu ,kulia ni Afisa mahusiano wa mfuko huo Bw.Abdul Njaidi akifatiwa na meneja Masoko na Mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah Keiya pamoja na Meneja Biashara wa kituo hicho Bi.Angela Maina
Kampuni ya Tana Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5  pamoja na mfuko wa kijamii wa PSPF imewafikia wadau wa mfuko huo kwa kuwapa elimu kupitia kipindi cha “Good-Morning Tanzania
Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Bw.Adam Mayingu akiongozana na Afisa mahusiano wa mfuko huo Bw.Abdul Njaidi walipokelewa na meneja Masoko na Mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah Keiya pamoja na Meneja Biashara wa kituo hicho Bi.Angela Maina
Akizungumza katika kipindi hicho kinachorushwa na kituo hicho Bw.Adam alisema kuwa ni wajibu wao kutoa elimu kwa jamii ili iweze kupata fursa ya kufahamu vema mfuko huo pamoja na kufaidika na huduma za afya za PSPF kupitia NHIF
Kwa upande wake Meneja masoko na mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah alisema uwepo wa mifuko ya kijamii inawezesha wananchi kupanga maisha yao ya sasa na baadae  na ndio maana Radio 5 imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mipango ya mifuko hii inawafikia walengwa
Bi,Sarah alisema kuwa Mkurugenzi wao Bw.Robert Francis amekuwa akiwezesha idara yao ya masoko na biashara kwa kutoa bei nafuu ya matangazo kwa mifuko hii ya kijamii ili kuwezesha kuwafikia wananchi kwa wingi na urahisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...