Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais leo Novemba 12, 2015
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Obeni Sefue alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
   Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati akiongea kabla ya kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais  Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiiangalia kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi aliyoipokea kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
 Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi  baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi  Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015
Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi  Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015.




TAARIFA YA MAKABIDHIANO  RASMI YA OFISI IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, leo katika Ikulu ya Dar es Salaam  amepokea taarifa rasmi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo mchana  na kushuhudiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue  na Maafisa wa  Ofisi Binafsi ya Rais.
Utaratibu wa kukabidhiana Ofisi katika Ofisi Kuu hapa nchini ni jambo la kawaida na hivyo imebidi  makabidhiano hayo  kati ya Rais anayeondoka na anaye ingia madarakani kufanyika.
“Umeanza vizuri, baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi” .  Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne amemueleza Mhe. Rais Magufuli wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
Mhe. Rais Mstaafu amekabidhi taarifa rasmi yenye kurasa 53, ambayo kwa ujumla inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika, ambazo zinasubiri kukamilika na zile ambazo zinasubiri maamuzi ya utekelezaji. Mengine ni  hali halisi ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  kwa muongozo wake siku zote .“Nikushukuru kwa kuiacha nchi salama na itaendelea kuwa salama, nikushukuru kwa muongozo wako, na  taarifa ya muelekeo na ninaahidi kuwa Hapa ni Kazi Tu”. 
 Mhe. Rais amesema na kumueleza Rais Mstaafu kuwa ametengeneza mazingira mazuri ambayo nchi nyingi zimeshindwa kufanya na hivyo basi kuahidi kuendelea kuchota hekima na busara kwa Marais wote wastaafu wakiwemo Mhe. Benjamin William Mkapa wa Awamu ya Tatu na Mzee Ally Hassan Mwinyi wa Awamu ya pili.
Wakati huo huo Mhe. Rais Magufuli ameendelea kupokea salamu za pongezi kutoka Kwa  Msimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bibi Helen Clark.
“Chini ya uongozi wako, tunatarajia kuzidi kuimarisha ushirikiano baina yetu, demokrasia, kushughulikia masuala ya umaskini na ajira kwa vijana , kukuza uchumi,  na kulinda na kuhifadhi mazingira, masuala ambayo Tanzania na UNDP tumekuwa tukishirikiana kuyaendeleza na kuyatimiza”  amesema Bi Clark.
Salamu zingine ni kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Uswiss, Mhe. Simonetta Sommaruga, Rais wa Jamhuri ya Italia Mhe. Sergio Mattarella, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Joachim Gauck na pia kutoka kwa Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto.
Pongezi zingine zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya Urusi, Mhe. Vladimir Putin, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Park Geun-hye na kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. XI Jinping.
Salamu  pia zimemfikia Mhe. Rais Dkt. Magufuli kutoka kwa Rais wa  Taifa la Eritrea Mhe. Isaias Afwerki na kutoka kwa Rais wa Ufaransa Mhe. Francois Hollande.Katika ujumbe wao, viongozi hao mbali na kumpongeza Mhe. Rais Dkt.  Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  wamesisitiza kuendeleza na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao.
Pia wameipongeza Tanzania kwa kudumisha demokrasia imara na Watanzania kwa ujumla kwa kuimarisha amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

12 Novemba, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hongera Jakaya, no where in the world does that happen. Huo ni uungwana wa hali ya juu.

    I cannot wait to see his Ministers doing the same.

    ReplyDelete
  2. Dear Rais,
    Uliwaahidi watz mabadiliko. Sasa unasema tena utachota hekima za wazee hawa. Ukifanya hivyo hakuna mabadiliko kwani utakuwa unadumisha mawazo yaleyale ya kale yaliyotufanya tutambae kimaendeleo.

    Kama unamaanisha madiliko lazima uwe na mapinduzi ya mawazo na hekima na hata ilani uipite katka utekelezaji. Watz wanahitaji zaidi ya ilani. kazi tuu lakini kwa mtazamo tofauti sio ile mitazamo ya kizamani.

    wakati nlikuwa nahisi wewe ndo tuliyekuwa tunamtafuta, usipochunga utaongoza miaka mi 5 tuu kwani watz wamechoka na kutokuwa na maendeleo.

    ReplyDelete
  3. Kikwete kakimbia tatizo la znz. We nawe unalifumbia jicho na kuziba sikio. Ujuwe wewe ni raisi. Na ulinadi uadilifu. Maana yake kumpa haki mwenyewe hata kama huna hisia nzuri kwake.

    ReplyDelete
  4. Ya wazanzibari nadhani waachiwe wenyewe, siasa za kule mie sizielewi kabisa kabisa, Maalim Seif anaenda kwenye mkutani yeye peke yake! hakuna mwenzake kutoka CUF na akitoka huko hana cha maana anachokisema zaidi ya kusema yeye mshindi atatangazwa! huku tunaona gazeti la serikali likitoa tamko rasmi la kuvunja muungano ETI tarehe Nov, na limetoka siku moja tu baada ya Seif kukutana na watu wa CCM ikulu ya Zenji! kuna nini kinaendelea! Maalim anawacheza shere wazaznibar ! so naona Rais wetu mtukufu sana Magufuli aachiwe afanya Kazi tu! kule awaachie wenyewe watatatua!

    ReplyDelete
  5. Rais Magufuli , kwanza , nikupe hongera . Tambua kwamba pamoja na ukweli kwamba hivi sasa wewe ni Rais wa watanzania wote , lakini usisahau kwamba asilimia 40%(approxy.)ya watanzania waliopiga kura hawakukuchagua/hwakukupigia kura .
    Ninacho kuomba , miaka mitano ya uongozi siyo mingi . Mwaka wa kwanza muda mwingi utautumia kujipanga na kupanga safu yako ya uongozi . Mwaka wa tano muda mwingi utautumia kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mwingine wa 2020 . Kwa hiyo , hakika utakuwa na miaka mitatu tu ya "Hapa ni Kazi Tu". Siyo mingi ukilinganisha na ahadi lukuki ulizozitoa kwa watanzania wakati wa Kampeni .
    Ili uweze kufanikiwa , na mimi nakuombea ufanikiwe ili uchaguliwe tena mwaka 2020 , nakuomba chondechonde , simama kama wewe Magufuli katika uongozi wako ,usije ukatumbukia katika mtego wa kutaka ushauri kwa wenzako waliokutangulia kila utakapo kwazwa na jambo . Simama kidete , fuata , tekeleza unayoyaamini , waliopita nao walipata muda wao wa kuonyesha uhodari wao.
    Katiba Mpya usiifumbie macho. Unaweza kuanza kwa kuirekebisha sheria inayosimamia Tume ya Uchaguzi , na suala zima la Katiba mpya likanyika polepole na kwa umakini mkubwa . Pitia safu nzima ya Viongozi serikalini , na kuwaweka kando wote waliopachikwa katika nafasi hizo "kama zawadi" bila ya kuwa na sifa stahili , wakuu wa mikoa , wakuu wa wilaya , wakurugenzi wa miji na majiji , wakurugenzi wa wilaya , makamishina wa idara za serikali nk.Utagundua nafasi hizo nyingi zitahitaji watu wenye taaluma ya sheria au uchumi au menejimenti . Lakini wapo madaktari , wanajeshi , makada wa chama , wapiga debe wa viongozi wa kisiasa , nk , walioshika nafasi hizo kama zawadi . Tunasubiri busara zako katika hilo . Watanzania wamechoka kubebebeshwa mzigo wa gharama ya serikali yenye mawaziri utitiri , wasio na tija yoyote .Baraza la mawaziri liwe dogo , ikiwezekana hata mawaziri 15 tu .jitahidi "Majorcracy" demokrasia ya wengi wape , iwe , "democracy" ya kweli , itakayo hakikisha haki kwa wote na ushiriki wa wote katika kufikia maamuzi yenye maslahi kwa wote au taifa zima . Nakutakia safari njema katika uongozi wako wa miaka mitano , ingawa hivi sasa imeshabakia miaka minne na miezi kumi hivi ! najua utaweza , usituangushe !

    ReplyDelete
  6. Hongera "press" ya Ikulu kwa kuongeza hadhi ya Ofisi ya rais kwa kuwa na e-mail address hiyo; sio tena ya bure ya google!

    Rais Magufuli, kabineti yako bado ni kubwa sana (bloated) ipeleke gym na kupunguza unene iwe na wizara 15 tu, kama ifuatavyo:

    1. Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
    2. Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi.
    3. Habari, Utamaduni na Michezo.
    4. Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
    5. Ulinzi na JKT.
    6. Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; na Sheria (Katiba na Utawala Bora).
    7. Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto.
    8. Afya na Ustawi wa Jamii.
    9. Mazingira, Nishati, Madini na Miundombinu.
    10. Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana.
    11. Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika.
    12. Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko).
    13. Kilimo, Ushirika, Uvuvi na Mifugo.
    14. Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge; na Mambo ya Ndani na Uhamiaji.
    15. Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia.

    ReplyDelete
  7. We ulietengeneza hizo wizara hujui uchambuzi. Elimu na sheria? Hilo limetinia shaka kuhusu hata kufikiria wazo lako.

    Mdau.

    ReplyDelete
  8. Mh Ris tunaomba utizame pia mgodi pekee wa Watanzania STAMIGOLD Biharamulo hasa kuuwezesha kiuchumi ili uweze kuendelea kusimama na kuipeperusha bendera duniani kote kuwa watanzania kuendesha migodi tunaweza bila kuwepo wazungu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...