Rais Jakaya Kikwete ateta na makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Maalim Shariff Seif Hamad kuhusu hali ya kisiasa
Visiwani leo asubuhi Ikulu jijini dar es Salaam
Wakiwa katika picha ya pamoja.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumatano,
Novemba 4, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Civic
United Front (CUF), Mheshimiwa Seif Shariff Hamad ambaye pia alikuwa Mgombea
Urais wa Zanzibar wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika
Oktoba 25.
Viongozi hao wawili walikutana kwa kiasi
cha saa moja Ikulu, Dar es salaam,
kuzungumzia hali ya kisiasa Zanzibar kufuatia ombi la Mheshimiwa Hamad kutaka
kukutana na kuzungumza na Rais Kikwete.
Viongozi hao wamekubaliana kuwa
mashauriano yaendelee kufanyika baina ya pande zote zinazohusika na hali ya
kisiasa Zanzibar.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba,
2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...