JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA
TAARIFA
KWA UMMA
UTEUZI
WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kipindi cha
miaka miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Oktoba 2015.
Uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu
Na. 9 (4) (a) cha Sheria Na. 20 ya Mwaka 1993 iliyoanzisha Kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL). Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette amekuwa Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia tarehe 13 Aprili
2005 hadi tarehe 13 Aprili 2015. Pia amekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, kwa taaluma ni Mhandisi ujenzi aliyobobea kwenye maeneo ya Mazingiria,
TEHAMA, Utawala na Menejimenti kwa zaidi ya miaka 25 na amesoma Vyuo Vikuu vya
Dar es Salaam, Tanzania; IHE Delft, Netherland; na Chuo Kikuu cha London,
Uingereza kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu. Pia ameshirikiana
na Vyuo Vikuu mbali mbali duniani kutoka Bara la Ulaya, Amerika, Asia na Afrika
katika maeneo ya uhandisi, utafiti, TEHAMA, uandishi wa vitabu na majarida
mbali mbali.
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...