Baada ya kulihutubia na kulizindua bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt JOHN POMBE MAGUFULI amehudhuria hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya wabunge katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma na kuagiza fedha zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla hiyo zipelekwe Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda vya wagonjwa.

Mheshimiwa Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa wadau mbalimbali wamechanga kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla hiyo ya wabunge katika siku ya uzinduzi wa Bunge.

Dkt Magufuli amesema alipata taarifa za kuwepo kwa michango hiyo ya fedha na kutoa maelekezo kuwa zitumike kwa kiasi kidogo kwa ajili ya hafla hiyo na sehemu kubwa zipelekwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili zikatumike kununulia vitanda na hivyo kupunguza tatizo la wagongwa wanaolala chini kutokana na uhaba wa vitanda unaikabili hospitali hiyo.

“Nilipoambiwa kwamba zimechangwa shilingi milioni 225 zimekusanywa kwa ajili ya sherehe, nikasema fedha hizo zipelekwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda” alisema Dkt Magufuli na kusisitiza kuwa “kwa kufanya hivyo tutakua tumejinyima sisi wenyewe lakini tutakua tumewanufaisha wenzetu ambao wanamatatizo makubwa yanayoweza kutatuliwa kwa fedha hizo”.

Awali akitoa taarifa ya michango hiyo Ofisa wa Spika wa Bunge Bwana SAID YAKUBU amesema jumla michango iliyopatikana na shilingi milioni 225 na kwamba fedha zilizotumika katika hafla hiyo ni shilingi milioni 24 tu baada ya kuzingatia maagizo ya Rais Magufuli.

Katika Hafla hiyo Rais Magufuli amekabidhi vyeti vya kutambua mchango wa wadau waliochangia fedha wakiwemo Benki za NMB, CRDB na Benki ya Afrika pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF na PPF.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU
November 20, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Msimamo huo huo, wasianze kujipendekeza hao.

    Hizo fedha zitakuwa na manufaa zaidi huko ulikopendekeza kuliko kuziishia na bia na soda.

    ReplyDelete
  2. 5 bila kabla ya half-time

    ReplyDelete
  3. That is what Tanzania needed! A leader who can make tough decisions that are of benefit to the regular Mwananchi

    ReplyDelete
  4. Mungu Hakupe maisha marefu mheshimwa rais wetu mpendwa.Ihitaji kuwa professor elimu kubwa ya juu inahitajia moyo wa kibinaadamu kuwafikiria na wengine walio chini yetu vipi wengine wanashindwa kuwafikiria wengine na kujijari wao tu.Hakika wapo wachache wa kariba kama yako na upatikana kila baada ya miongo kadha tusipokutumia sasa kumpata mbadala wako itatuchukua miongo mingine kadha.

    ReplyDelete
  5. Kwa mara ya kwanza tamgu nizaliwe naanza kupata matumaini na raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania

    ReplyDelete
  6. Haya ndio mambo yanayotakiwa kufanya kwa mwanadamu mwenzako, hili ni Taifa litajengwa na mwananchi mwenyewe, mwananchi ni yoyote yule. Mwenye mapenzi mema

    ReplyDelete
  7. This is what I've been waiting to see in my country.waiting for more to come...

    ReplyDelete
  8. Huyu ndiye JPM niliyemjua siku zote, haionekani kama atabadilika. Daima kazi kazi

    ReplyDelete
  9. Tunamuombea Rais JP Magufuli afya njema na maisha marefu awatimizie wanyoge.

    wa Tanzania tujifunze kujitolea kwa Hali na Mali kwa faida ya wasio na uwezo Mhe JPM ameonesha mfano, tusijitie viziwi na vipofu...
    Twende na msimamo wake na utekelezeji wake.

    Abarikiwe...

    ReplyDelete
  10. The hope for my country has been rekindled after the incredulous death of Moringe Sokoine(RIP). Unfortunately the load is too heavy for JPM to carry it alone. At the moment I am suspecting that Tanzanians are in shock at the possibilities that one person can bring. I edge my fellow citizens, instead of waiting for his excellency JPM to do everything, we need to lend him a hand to him in our capacities not matter how small or insignificant by being proactive in doing good for ourselves, our nation and specifically our children. Every developed nation on Earth was built by its own citizens. There is no nation that was built by foreigners and prospered. We, as Tanzanians should come first in everything we do and plan; we have to seize the opportunity before detractors seize it again. Once again I remind every Tanzanian of goodwill, Magufuli can not and will not do it alone, he needs a lot of hands coming together to embrace the cause. Prayers alone are not enough. Please go out, do something for yourself and someone else. It is very sad to live in such a rich country like mine i.e. Tanzania, but we citizens are poor; while every foreigner sees opportunity. God has given us a second chance, however it took almost a generation for a gutsy leader to come about. Whether it is luck, or God sent, let us do our part, then Magufuli will be fine.

    ReplyDelete
  11. Welldone mheshimiwa...kwa mwendo huu utaondoa u selfish kwa watanzania.....na utaweza kujenga tanzania mpya....msio wajua wasukuma hawa ndio watanzania walio bakia pekee wasio ma selfish very nice people ....wasiokuwa na tamaa na chochote god bless tz

    ReplyDelete
  12. This is a person leading other people. The task is for us the citizens to appreciate and do our little parts to make this great nation really great!!! we have a great nation and leaders can make such a different, if only we could get five of this kind. God bless the president JPM and may God bless Africa and Please God bless Tanzania. We have waited long enough for this kind of hope!!!
    A person's humanity is weighed by how he treats other fellow human beings, selfless is most self satisfying than selfishness, if all leaders could understand this!!!!

    ReplyDelete
  13. Hongera rais kwa kuliona hilo mungu akupe ujasiri wwa kutenda yale uliyo tuhaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...