NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MKUU WA Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) mkoani hapa kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa
wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuweza kuongeza
wigo mpana wa wanachama ambao wataweza kunufaika na huduma zao.
Alitoa wito huo jana wakati akipokea mashuka 150 yaliyotolewa na mfuko
huo vyenye thamani ya shilingi milioni tatu yaliyotolewa na Mfuko huo
kwa ajili ya vituo vitatu vya afya vya Mkinga, Maramba na Lanzoni
vilivyopo wilayani Mkinga ambavyo zilikuwa zikikabiliwa na changamoto
ya uhaba wa mashuka.
Kwa upande wake, Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani
Tanga (NHIF) Ally Mwakababu alimueleza Mkuu huyo wa mkoa kuwa dhamira
yao kubwa ni kuhakikisha wanasaidia huduma za afya kwenye maeneo
yalikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa mashuka.
Aliongeza kuwa mikakati yao ni kuongeza ufanisi mkubwa katika
kuwahudumia wananchi waliojiunga na mfuko huo ili waweze kupata huduma
za uhakika wakati wanapokuwa kwenye vituo vya afya ili kuepukana na
usumbufu usiowa wa lazima
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza akipokea mashuka 150 kutoka kwa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga,Ally Mwakababu kwa ajili ya vituo vitatu vya Afya,Maramba,Mkinga na Lanzoni vilivyopo wilayani Mkinga mkoani hapa,Picha na Oscar Assenga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) mkoani Tanga ofisini kwake mara baada ya kupokea mashuka 150 kwa ajili ya vituo vitatu vya Afya,Maramba,Mkinga na Lanzoni vilivyopo wilayani Mkinga mkoani hapa kulia ni Meneja wa NHIF mkoa wa Tanga,Ally Mwakababu na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Salum Chima na anayefuatia ni Afisa Matekelezo wa (NHIF) Miraji Msile.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...