Kampuni ya Bima za Afya ya Resolution leo hii iliandaa tamasha maalum la wanamazoezi wa wilaya ya Kinondoni lililofanyika katika Viwanja Vya Leaders Club. Tamasha hilo lilihudhiriwa na umati wa watu wengi wanaofanya mazoezi ya kukimbia taratibu kwa afya maarufu kama “Jogging”.

Wakimbiaji katika maeneo mbalimbali jijini Dar Es Salaam hujiunga kwa pamoja na kuanzisha vilabu vyao kwa lengo la kufanya mazoezi haya kwa pamoja. Vilabu hivi maarufu kama “Jogging Clubs” husaidia kuhamasisha wajumbe wake sio tu kuhudhuria mazoezi kwa ratiba iliyopangwa lakini pia kuishi maisha yanayojali afya zao.
 Akizungumza katika Tamasha hili la vilabu mbalimbali vya wakimbiaji wa wilaya ya Kinondoni, Bwana Oscar Osir, Meneja mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution alisisitiza kwamba kampuni yake imedhamiria hasa kuwafahamisha wananchi wote kuhusu uchaguzi wa aina ya maisha yanayojali afya zao. 

Aliendelea kusema, “Mjumuisho wa kufanya mazoezi mara kwa mara na kula chakula bora ni muhimu sana katika nyakati hizi ambapo tunaandamwa na maradhi mbalimbali. Kampuni yetu iko mstari wa mbele na tutafanya kila linalowezekana kuwawezesha wananchi kuishi maisha bora kadiri wawezavyo”.

Bwana Osir alimalizia kwa kusema kwamba, “Tamasha hili ni mwanzo tu wa jitihada zetu kukutana na wananchi na kuhamasisha ufanyaji mazoezi na kuzingatia ulaji wa chakula bora, hatuishii hapa, tunategemea kukutana na wananchi wa sehemu nyingine mbalimbali katika siku za usoni.”
Naye Mwenyekiti wa vilabu vya wakimbiaji wilaya ya Kinondoni Bwana xxx xxx alitoa shukrani nyingi kwa kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution kwa kuwathamini na kuandaa tamasha hilo. 

Alitoa wito kwa wananchi mbalimbali kujitahidi kutenga muda wa mazoezi japo mara moja kwa wiki. Alimaliza kwa kusema , “Mazoezi hukufanya ujisikie vizuri siku nzima, pamoja na kuboresha afya yako mazoezi pia hupunguza msongo wa mawazo, tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi siku hizi.” Aliwaasa wananchi kujali afya zao mapema, wajiunge na vikundi vya Jogging popote walipo.
Wafanya mazoezi mbalimbali kutoka Wilaya Kinondoni wakiwa katika mazoezi maeneo ya barabara ya Kawawa wakielekea Leaders Klabu kumalizia mazoezi yao ikiwa ni sehemu ya kuihamasisha jamii kufanya mazoezi yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution Insurance Dar es Salaam jana.
Mwalimu wa mazoezi akiwaongoza wafanya mazoezi kutoka Wilaya ya Kinondoni kufanya mazoezi yaliishia kilele chake katika viwanja vya Leaders Klabu yenye lengo la kuihamasisha jamii kufanya mazoezi kwa udhamini wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution Insurance Dar es Salaam jana.
Wafanya mazoezi mbalimbali kutoka Wilaya Kinondoni wakiwa katika foleni ya kupima afya zao mara baada ya mazoezi kumalizika ikiwa ni sehemu ya kuihamasisha jamii kufanya mazoezi yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution Insurance Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...