MWIMBAJI mahiri wa muziki wa
Injili Afrika Mashariki na Kati, Ephraim Sekeleti amethibitisha kuwa
mmoja wa waimbaji watakaopanda jukwaa la Tamasha la Krismasi na
kushukuru linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Sekeleti amekubali kuwa
mmoja wa waimbaji wa Kimataifa watakaopanda jukwaa la Shukrani ambalo
litakuwa katika Sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa Masia, Yesu Kristo.
Msama alisema tamasha hilo ni la
Shukrani baada ya kuombea amani uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25,
Tamasha la Maombi lilifanyika Oktoba 4 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
“Tunarudisha heshima na Shukrani
kwa Mungu baada ya kuiepusha Tanzania na majaribu yaliyokuwa na mlengo
wa kutaka kuvuruga amani ambayo iliasisiwa na baba wa Taifa Mwalim
Julius Kambarage Nyerere,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema kuandaa
tamasha hilo inaonesha namna gani Watanzania tulivyo na shukrani ambako
Watanzania tukumbuke kwamba Tukipewa, Tusisahau kushukuru.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...