Serikali imeamua kutoa elimu pasipo malipo kwa elimu ya msingi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne, kuanzia mwaka wa masomo wa 2016 kama ilivyoahidi. 
 Azma hii ya serikali ni katika kutekeleza sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania wanapata Elimu bila kikwazo ikiwemo ada au malipo. 
 Katika kutekeleza maamuzi hayo, ada zote zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne zimefutwa.
Pia, waraka wa Elimu namba 8 wa mwaka 2011 kuhusu michango shuleni nao pia umefutwa.
 Aidha, mwongozo wa elimu ya msingi bila malipo unaandaliwa na utatumwa kwa wamiliki wa shule ifikapo au kabla ya tarehe 15 Disemba 2015. Waraka huu umeanza kutumika tarehe 21 Novemba 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...