DSC_1839Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akizungumza mbele ya wanahabari, madaktari na baadhi ya akina mama waliokuwa na watoto waliozaliwa kabla ya wakati maarufu kama Njiti (Hawapo pichani). Kushoto ni DoriS Mollel ambaye ni Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) na wengine ni maafisa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale, Modewjiblog
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongeza juhudi binafsi zinazofanywa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) katika harakati zake za kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) na mambo ya elimu hapa nchini huku ikiahidi kuendelea kushirikiana nayo kufikia malengp yake.

Kauli hiyo imetolewa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki wakati wa kupokea vifaa maalum vya kusaidia watoto njiti vilivyotolewa na taasisi hiyo ya Doris Mollel Foundation tukio lililofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jengo la Watoto.

“Tunatambua mashine hizi ni bei kubwa na Serikali pekee yake haina pesa hivyo kwa kusaidiana na wadau kama hivi n faraja sana na tunapongeza juhudi hizi za taasisi ya DMF kwa kujitokeza kusaidia mashine kwa watoto njiti” ameeleza Mkuu wa Mkoa huyo.

Mkuu wa Mkoa huyo aliongeza kuwa, Mashirika mengine yaendelee kujitokeza kusaidia huduma za kijamii ikiwemo vifaa kama taasisi ya Doris Mollel kwani asilimia 100 ya wagonjwa na watu wengine wenye mahitaji katika tiba wanakimbilia Dar es Salaam hasa Hospitali ya Muhimbili.

“Tunaomba tena mukipata nyingine musisite kutiletea hapa maana Mkoa huu unapokea wagonjwa wengi kutoka maeneo mengi ya Tanzania na vifaa vya tiba mara nyingi vinakuwa ni vichache, Huko mikoani wanapewa rufaa waanakuja hapa pia hivyo DMF musisite kuja tena” alimalizia Mkuu wa Mkoa huyo.

Hata hivyo kwa upande wake Mwanzilishi na mtendaji Mkuu wa DMF, Doros Mollel amemweleza Mkuu wa Mkoa Meck Sadik kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega katika juhudi za kusaidia watoto njiti nchini ikiwemo kutoa elimu, vifaa na usaidizi kwa jamii dhidi ya kukabiliana na watoto njiti nchini.

Katika tukio hilo, Mkuu wa Mkoa alishudia vifaa hivyo na kupokea kutoka DMF sambamba na kutembelea wote ya watoto njiti pamoja na ile ya Kangaroo ambayo wamama wenye watoto njiti wanakuwa wanapatiwa uangalizi maalum dhidi ya watoto wao ikiwemo kupata joto la Mama na baadae alipanda mti maalum mbele ya jengo hilo la Watoto kama kumbukumbu na juhudi za wadau katika kusaidia jamii dhidi ya watoto njiti.

DMF imeweza kusaidia vifaa katika wodi hiyo ya watoto Muhimbili vikiwemo (Suction machines, Oxygen Concentrators na Feeding tubes). Aidha Doris Mollel amebainisha kuwa baada ya hapo wanatarajia kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoa vifaa kama hivyo huku lengo ikiwa ni kufika mikoa yote ya Tanzania.
DSC_1855
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo maalum la taasisi ya DMF ilipotoa vifaa hivyo katika kitengo cha Jengo la Watoto.
DSC_1865
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik akipata maelezo juu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Taasisi ya DMF.
DSC_1870
Msimamizi wa wodi ya akina mama wanaopatiwa huduma ya Kangaroo dhidi ya watoto wao ambao walizaliwa njiti, akimpatia maelezo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipotembelea wodi hiyo leo.

BOFYA HAPA WA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. HONGERA BINTI MWENYEZI AKUBARIKI AKUZIDISHIE PALE ULIPOTOA KWA KUJALI WATOTO NJITI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...