Mkulima wa karafuu wilaya ya Wete akionyesha matawi ya mkarafuu
yaliyokatwa na wezi shambani kwake kwa lengo la kuiba karafuu.
Na Ali Mohamed
SERIKALI imepiga marufuku uuzaji na ununuzi wa karafuu usio rasmi (vikombe) kuepusha wizi wa karafuu mashambani na ukataji wa mikarafuu unaofanywa na baadhi ya watu kutokana na kuzoeleka kwa biashara hiyo.
Wakizungumza katika nyakati tofauti Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba wamesema hakuna ruhusa kwa mtu yoyote kuuza au kununua karafuu mbichi au kavu na atakaebainika kujihusisha na biashara hiyo atashughulikiwa ipasavyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla alisema tatizo la ununuzi wa karafuu kwa vikombe, wizi na ukataji wa mikarafuu kwa lengo la kuiba karafuu lipo.
Alibainisha kuwa Serikali haiwezi kuvumilia makosa hayo kwa sababu wanaofanya uhalifu huo hawana imani na Serikali haina imani nao. Alifahamisha kuwa watakaokamatwa watachukuliwa hatua kwa misingi ya kisheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...