Katika mkakati wake wa kukuza ujasiriamali na ubunifu wa miradi endelevu nchini,Benki ya Stanbic imedhamini shindano la Seedstars World kwa ajili ya wajasiriamali wenye mawazo ya miradi endelevu ambalo limefanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kwenye shindano hilo kampuni ya Juabar imeibuka na ushindi wa kushiriki kwenye shindano la ngazi ya kimataifa litakalofanyika nchini Uswisi mwezi Februari mwakani ambapo itawania kitita cha Dola za Kimarekani 500,000 kwa ajili ya kufanikisha uwekezaji inaotarajia kuufanya. Na gharama za ushiriki zitagharamiwa na Benki ya Stanbic.
Wazo la mradi wa kampuni ya Juabar ni kuanzisha teknolojia ya kusambaza vifaa vya kuchaji simu za mkononi kwa kutumia umeme wa jua ambapo vifaa hivyo maalumu vitasambazwa kwa watumiaji wa simu kwa gharama nafuu na kuwapunguzia adha wanayoipata kupata huduma hiyo kutokana na matatizo ya nishati ya umeme yaliopo hapa nchini.
Akiongea kuhusiana na shindano hili kwa wajasiriamali Mkuu wa Kitengo cha huduma za biashara wa Benki ya Stanbic Tanzania Bw.Christopher Mlay amesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa kuendeleza wafanyabiashara hususani wajasiriamali kwa ajili ya kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.
Alisema Benki ya Stanbic imejipanga kuwaendeleza wafanyabiashara nchini ambapo imebuni huduma mbambali za kuwaendeleza na inafurahi kushirikiana na wadau mbalmbali wenye dhamira ya kukuza ujasiriamali na ubunifu wa miradi yenye tija inayoweza kuleta mafanikio kwenye jamii kama lilivyo shindano hili la Seedstars World.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kampuni ya Juabar,Olivia Nava amesema anajivunia ushindi huo kupitia wazo la mradi wa nishati ya umeme wa jua na ana Imani itafanya vizuri kwenye shindano la kimataifa.
Shindano la Seedstars World linazidi kupata umaarufu mkubwa kwa kusaidia kuendeleza wajasiriamali kutoka nchi mbalimbali duniani.Mwaka jana lilishirikisha makampuni ya ujasiriamali 36 ambapo mwaka huu itakutanisha wajasiriamali 53 nchini Geneva,Uswisi pia shindano hili limekuwa likilenga kuendeleza ubunifu wa matumizi ya teknolojia kwa makampuni machanga.
Kwa maelezo zaidi tembelea:
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...