Katika
kufikia ahadi yetu iliyopo kwenye malengo
na dira ya benki ya kuwa taasisi ya
fedha inayopendelewa zaidi nchini kupitia mtandao mpana wa matawi unaotoa
huduma kwa gharama nafuu zaidi zenye kumlenga mteja na jamii ya watanzania,
Tunapenda
kuwataarifu wateja wetu na umma kwa ujumla kuwa matawi yetu yote yatafungwa
siku ya Alhamisi Novemba 5, 2015 ili kupisha sherehe za kitaifa za kuapishwa
kwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa
Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Huduma zitarejea tena katika matawi
yetu yote siku ya Ijumaa Novemba 6, 2015 kuanzia saa 2:30 asubuhi.
Ili
kuhakikisha kuwa tunaendelea kukupatia huduma bora siku hiyo, njia mbadala za kibenki
kama ATM, NMB mobile, NMB Wakala na Internet Banking zitaendelea kufanya kazi kama
kawaida kwa masaa 24.
Hata
hivyo, kituo chetu cha huduma kwa wateja kitaendelea kuwa wazi mpaka saa 2:00
usiku. Hivyo unaweza kuwasiliana na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa
kupiga simu ya bure 0800 11 22 33 kwa
msaada zaidi.
Imetolewa na Menejimenti ya NMB
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...