Mheshimiwa Wilson M. Masilingi,
Balozi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania nchini Marekani, anasikitika
kutangaza kifo cha Bi. Nyamiti Ivan Lusinde, aliyekuwa mfanyakazi wa Ubalozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington DC.
Bi. Nyamiti Ivan Lusinde alifariki dunia Jumanne tarehe 17 Novemba,
2015 Dar Es Salaam, Tanzania ambapo alikuwa likizo yake ya mwaka.
Kitabu cha rambirambi kipo
nyumbani kwa marehemu
20408
Honey Crisp Lane, Apartment E
Germantown,
MD 20876
Maelezo zaidi kuhusu taratibu za
mazishi
yatatolewa mara baada kupokea taarifa zaidi kutoka nyumbani Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...