Mama Euphrazia Gillian Ntukamazina anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake, Mwalimu Leah Chabakanga (pichani) kilichotokea Jumapili tar 8 novemba 2015 katika hospitali ya TMJ Jijiji Dar es salaam.
Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu inafanyika nyumbani kwa Bw Deogratias Ntukamazina, Mbezi beach tangi bovu.
Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki walioko Dar es salaam, Ngara, Musoma, Mwanza na Arusha.
Ratiba: kutakuwa na misa ya kumuombea marehemu siku ya Jumatano tar 11 novemba 2015 katika Kanisa la KKKT Mbezi tangi bovu kuanzia saa 9 alasiri na baada ya hapo safari ya kuelekea Ngara kwaajili ya mazishi itaanza asubuhj ya alhamisi tar 12.
Mungu aiweke Roho ya Mareheu Mahala pema Peponi
-Amin.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...