Mgeni rasmi katika Tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani
lililoandaliwa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation (DMF), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa kwenye meza kuu na Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Anna Mgwhira (kushoto), Mkurugenzi wa Hunduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila (kulia) pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel, wakati wa muendelezo wa tamasha hilo lenye lengo la kufanya harambee kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa vifaa maalum vya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo. Kilele cha kumbukumbu hiyo ya mtoto njiti Duniani kinatarajiwa kufanyika Novemba 17, 2015.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika Tamasha la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lililoandaliwa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation (DMF), lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo. Akitoa hotuba yake, Makonda amesema kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali ili kuhakikisha watoto njiti wanapata huduma stahiki katika mazingira rafiki ili waweze kuishi kama watoto wengine.

Mwenyekiti wa chama cha (ACT) Wazalendo, Anna Mgwhira ambaye alikuwa ni mmoja wa wageni waalikwa, akizungumza katika Tamasha hilo la kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo
Mkurugenzi wa Hunduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila akizungumza katika hilo, lilifanyika kwenye Viwanja wa Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.

Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akizungumza wakati akitoa shukrani kwa wadau mbali mbali waliolifanyikisha Tamasha hilo kwa namna moja ama nyingine.

Sehem ya wadau mbali mbali na wananchi waliofika katika tamasha la
kuelekea kumbukumbu ya siku ya mtoto njiti Duniani leo katika viwanja
vya Leaders Clubu jijini Dar es Salaam
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...