Ubalozi wa Marekani
 Dar es Salaam
TANZANIA
5 Novemba, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa niaba ya Rais Obama na watu wa Marekani, nawapongeza watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uchaguzi wa rais na wabunge ulioendelea kuthibitisha rekodi nzuri ya Tanzania katika kujenga demokrasia imara.
Wakati Rais John Pombe Joseph Magufuli na serikali yake wakichukua majukumu yao, tunatarajia kuendelea na ubia wetu wa karibu na kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya nchi zetu mbili tunapofanya kazi pamoja ya kusaidia ujenzi wa demokrasia, kukuza usalama wa kikanda na kuendelea kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Aidha, napenda kumshukuru Rais aliyemaliza muda wake Jakaya Kikwete kwa jitihada zake za kujenga uhusiano imara na wa kudumu kati ya Marekani na Tanzania.
Hata hivyo, Marekani inaendelea kustushwa sana na tamko la mamlaka visiwani Zanzibar la kusudio la kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar wa Oktoba 25.
Kwa dhati kabisa, tunatoa wito kwa serikali mpya kuhakikisha kuwa maamuzi ya watu wa Zanzibar yanajidhihirisha  katika ukamilishwaji wa haraka, wa haki na wa amani wa mchakato wa uchaguzi visiwani Zanzibar.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tatizo kubwa la uchaguzi wa Zanzibar ni ongezeko la kura zilizopigwa huko Pemba kulinganisha na idadi halisi ya walioandikishwa kupiga hizo kura, pia vitisho vilivyokuwa vikipewa watu ambao walionekana kuwa sio wafuasi au wapiga kura wa chama fulani.
    Kwa bahati mbaya sana waangalizi wa kimataifa ambao wamekuwa na tarumbeta nyingi wao wanang'ang'ania kazi iendelee!!! Itaendeleaje katika hali iliyojaa dhulma kama hii?
    Sisi Wazanzibari na hasa tulio hapa Zanzibar (Unguja) wengi wetu hatukubaliani na hizo tarumbeta za akina Jussa na vibaraka wengine wa Sultani aliyepinduliwa na tutaendelea kuyalinda Mapinduzi yetu kwa gharama zozote.
    Tunataka uchaguzi unaoendeshwa kwa njia za halali.
    Hivi ongezeko la wapiga kura mbele ya hao vinyankela vinavyojiita jumuiya ya kimataifa haliwi tatizo kwenye uchaguzi? Mbona linapotokea Burundi au kwa vyama vingine tawala linakuwa ni ajenda?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...