Tabibu Gonzaga Marwa akiangalia baadhi ya mkopo ya Dawa jijini Dar es Salaam leo.
TAASISI
isiyo ya Kiserikali ya Tanzaone Herbal Clinic chini ya mradi wake wa ‘Tanzaone’
hatimaye imethibitisha pasipo shaka kuwa mmea ujulikanao kama Rozella na bidhaa
zitokanazo na mmea huo hazifai kwa matumizi ya binadamu na wanyama.
Akizungumza
na waandishi wa habari, sanjari na kuonyesha majibu ya vipimo vya kitaalamu
kutoka Wakala wa Maabara ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali kupitia utafiti
uliofanywa chini ya mradi huo, Mratibu wa mradi.
Tabibu Gonzaga Marwa,
amesema matokeo ya uchunguzi wa sampuli
za mmea huo yameonesha una ukuvi yaani ‘fangasi’ aina ya Aspergillus ambao
hutoa sumu ya Aflatoxin ambayo huweza kusababisha saratani ya maini.
Aidha,
Tabibu Marwa ameiomba serikali kupitia Wizara ya Afya, na Mamlaka ya Chakula na
Dawa TFDA, kuhakikisha wanachukua hatua za haraka kunusuru afya za walaji,
sambamba na kushauri wadau wa tiba asili nchini kufanya utafiti wa kina wa dawa
za mitishamba na bidhaa zake kabla ya kumfikia mlaji.
Hati ya uchunguzi
ya Mradi huo, namba 241/2013, uliopewa jina la ‘Tanzaone Red Tea Juice’ na
kudumu kwa miaka mitatu 2010/2013, kwa kushirikisha watuamiaji wakubwa wa
Lozera zaidi ya 250 nchini kote, ilichunguzwa, kuidhinishwa na kuthibitishwa na
Mkemia Mkuu wa Serikali
Mbali na kuongeza juhudi zinazochukuliwa na wavumbuzi na wajasirimali kutengeneza na kuuza dawa zitumiazo mime asilia, kuweza na Sheria ya ku chungu za na kupima dawa hizi kabla hazijaingizwa kwenye Soko.
ReplyDeleteKwa style hii tutakufa wengi TFDA wamekuwa wapi Siku zote lozera zauzwa supermarket,sokoni ukienda madukani,je ni vitu vingapi kama lozera tunatumia kumbe vinamadhara,tunaomba kama mkemia mkuu ameithibitisha hii TFDA wafanye him a kuilemisha jamii maana jamii kubwa itaangamia kwa kutokupata welewa.
ReplyDeleteNafikiri ni 'Rosella' siyo 'Lozera'
ReplyDeleteNadhani kwa kiswahili labda ndio hiyo 'Lozera' na kizungu au kitaalam yawezekana ndio hiyo 'Rosella' (Hibiscus sabdariffa Linn.) Ila ukitokezea pande za kwetu kule, mmea huu almaarufu kwa jina la 'Choya' na sana sana yale maua yake, lakini kila sehemu nadhani wana jina lake maalum tukiachana na hayo ya kitaalam. Sasa kama kuna madhara juu ya mmea huu khususan maua yake ndio zao kuu, basi naamini wataathirika wengi au hata wameshaathirika wengi, maana baadhi ya sehemu nimeshashuhudia wakiyatumia maua yake kutengenezea pombe za kienyeji, tena kwa njia za kienyeji na hili sio leo wala jana, ni dahari zilizopita kabla hata haujawa maarufu mmea huu kama ulivyokuja kuvuma miaka hii ya karibuni, kwa maana hiyo hao walioanza kuitumia Rozella/Lozera tangu miaka hiyo wamefanyiwa utafiti na wao au kuna kitu gani kilicho 'trigger' mmea huo na kupelekea kuonekana haufai kabisa kwa kila hali, ili elimu zaidi iendelee kutolewa ikibidi na matangazo katika vyombo vya khabari ili kuweza kuwafikia wengi uelewa na madhara ya Lozera/Rosella. Pia kama ndio kweli yameshabainika madhara yake ni vyema pia stock iliyopo kama ni madukani ama popote pale ikateketezwa ili kunusuru watumiaji wake wasije kuendelea kuathirika zaidi.
ReplyDeleteKupeaana habari ni muhimu lakini ninachokiona kuna ushindani wa uwezo wa mitishamba mingine na rozela kwa hiyo wataalamu wa mitishamba wanajaribu kukatisha tamaa matumizi ya rosella ili wapate wagonjwa wengi na wagojwa hao watawatibu kutumia rozela hiyohiyo lakini kwa jina linguine. Aflatoxin inapatikana zaidi ya mara 100 kwenye mahindi ukilinganisha na rozela, so nilitegemea msititizo ungekuwa kwenye kitu ambacho watanzania tunatumia zaidi na ni mra 100 zaidi ya kiwango kilichopo kwenye rosella. Lakini pia ipo zaidi ya mara 60 kwenye karanga (peanut) ukilinganisha na rozela. Karanga na mahindi vinatumika zaidi ya mara 10000 ukilinganisha na wanywaji wa juice a rosella kwa ajili ya kuongeza damu, vitamin A, B1, B2, B6 na C. Na ni msaada mkubwa kwa wajawazito ( IMEOKOA MKE WANGU Beatrice hii rozela that is why baada ya kuambiwa sumu imebidi niisome history, matumizi, viinitiba na madhara ya rozela).Nimegundua kwa rozela inakiwango kidogo cha kiinifungasi cha aflatoxin ukilinganisha na vyakula tunavyokula kila siku kama mahindi, karanga, maziwa, butter na mafuta ya pamba.Kiini hiki huathiri zaidi panya. Pombe ya rozela ndiyo yenye aflatoxin. Ukweli umebaki kuwa ROZELA inaongeza damu kwa haraka, inavitamini A,B na C. Nimesoma vingi, ebu na wewe soma kiambanisho kifuatacho:Aflatoxin Introduction
ReplyDeleteAflatoxin is a potent human carcinogen. It is a naturally occurring toxic metabolite produced by certain fungi (Aspergillus flavis), a mold found on food products such as corn and peanuts, peanut and butter. It acts as a potent liver carcinogen in rodents (and, presumably, humans). They are probably the best known and most intensively researched mycotoxins in the world. Aflatoxins have been associated with various diseases , such as aflatoxicosis , in livestock , domestic animals and humans throughout the world .
The occurrence of aflatoxins is influenced by the weather, (temperature, and humidity - warm & wet is worst!); so the extent of contamination will vary with geographic location , agricultural and agronomic practices, and the susceptibility of the peanuts (etc.) to fungus before they are harvested, and during storage, and/or processing periods . Aflatoxins have received greater attention than any other mycotoxins because they clearly have a potent carcinogenic effect in laboratory rats and their acute poisonous effects in humans .
In the 1960 more than 100,000 young turkeys on poultry farms in England died in the course of a few months from an apparently new disease that was termed "Turkey X disease" . It was soon found that the difficulty was not limited to turkeys . Ducklings and young pheasants were also affected and heavy mortality was experienced .
A careful survey of the early outbreaks showed that they were all associated with feeds, namely Brazilian peanut meal . An intensive investigation of the suspect peanut meal was undertaken and it was quickly found that this peanut meal was highly toxic to poultry and ducklings with symptoms typical of Turkey X disease .
Speculations made during 1960 regarding the nature of the toxin suggested that it might be of fungal origin. In fact, the toxin-producing fungus was identified as Aspergillus flavus (1961) and the toxin was given the name Aflatoxin by virtue of its origin (A.flavis--> Afla).
Evidence of acute aflatoxicosis in humans has been reported from many parts of the world , namely the Third World Countries. The syndrome is characterized by vomiting, abdominal pain, pulmonary edema, convulsions, coma, and death with cerebral edema and fatty involvement of the liver , kidneys , and heart.
Conditions increasing the likelihood of acute aflatoxicosis in humans include limited availability of food, environmental conditions that favor fungal development in crops and commodities, and lack of regulatory systems for aflatoxin monitoring and control( Avoiding mold and humidity in food).
Asante kwa shule, pombe ya Rosella wengine tumeshatumia sana yaani, tusubiri matokeo. Either ni kuacha kuendelea na matumizi hayo.
ReplyDelete