Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akihutubia Bunge la Jamhuri kama ishara ya kuzindua Bunge la 11.
Kabla ya Rais Dkt. Magufuli kuzindua Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju aliomba Bunge likubali kutenguliwa kwa kanuni za Bunge ili kuruhusu wageni kuingia ndani ya Bunge hilo.
Wabunge walionesha kuridhishwa na hotuba ya Mhe. Rais Makufuli, wakipiga meza kuunga mkono hotuba hiyo.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli (wa pili kushoto) akiwa na Marais Wastaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia), Benjamin Wiliam Mkapa (kulia) na Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kama unataka kukusanya kodi kwa wingi basi tumia electroniki. Hizo risiti ziandikwe na mashine na hiyo mashine iwe kwenye mtandao na kila mashine iripoti TRA mauzo ya siku, kila siku, automaticaly.

    ReplyDelete
  2. Hongera Mheshimiwa Rais kwa hotuba yako adhimu na iliyoelekeza matarajio ya Uongozi wako kwa miaka mitano ijayo. Mheshimiwa,kiu yangu kuu ni ya kihistoria ambayo ningependa kuona tunamuenzi baba wa Taifa letu Mwlm Nyerere kwa kuitekeleza ndoto yake alipotaka kuhamishia Makao Makuu ya nchi yetu kwenda Dododma. Hili litasaidia kwanza kuondokana na msongamano na maisha yasiyoyakiafya ambayo Watumishi wa mawizara na taasisi za Serikali wanalazimika kuishi ili kuweza kutekeleza majukumu yao. Si kuwa watu wanapenda kuishi maisha ya kiduni na yasiyo rafiki kiafya bali ni lazima sababu Serikali ipo Dar Es Salaam.

    Twende Dodoma baba!!

    Hili ni ombi na ushauri wangu binafsi.

    BNS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...