
KAMPUNI ya Total ya Tanzania, imezindua Shindano la Total «Startupper of the year by Total», lililobuniwa na kundi la Makampuni ya Total litakaloshirikisha nchi 34 za Afrika kwa wakati mmoja.
Shindano hilo linalenga katika kutambua, kuzawadia na kuwezesha utekelezaji wa miradi bora ya biashara ya ujasiliamali inayoanza au iliyobuniwa chini ya miaka miwili kwa ajili ya maendeleo ya jamii na taifa.
Shindano hilo linalenga katika kutambua, kuzawadia na kuwezesha utekelezaji wa miradi bora ya biashara ya ujasiliamali inayoanza au iliyobuniwa chini ya miaka miwili kwa ajili ya maendeleo ya jamii na taifa.
Washindi wa miradi bora watapewa tuzo ya « Startupper of the year 2016 by Total » itakayoambatana na fedha taslimu itakayotumika kama mtaji wa kuendeleza, na kusimamia uendeshaji wa miradi hiyo.
Shidano hili ni bure kwa raia wote wa Watanzania wenye umri kati ya miaka kumi na nane( (18) hadi miaka thelathini na tano (35).
Fomu za maombi zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 1 Novemba 2015 saa 2:00 asubuhi kwenye tovuti: http://startupper.total.com/. Shindano litakuwa wazi hadi Januari 31, 2016 saa 5:00 asubuhi ambapo ndio mwisho wa kurejesha fomu.
Jopo la Majaji linalohusisha wataalamu wa biashara, litachagua miradi kumi bora nchini Tanzania itakayoingia fainali kwa kuzingatia vigezo vya ubunifu, uhalisia na uwezo wa mradi katika kuleta maendeleo na kuboresha hali ya maisha ya jamii kubwa ya Watanzania.
Orodha ya washindi watakaoingia fainali itachapishwa tarehe 28, Februari, 2016 katika tovuti ile ile walipochukulia fomu za kugombea.
Kuanzia tarehe 15 Machi, 2016, Washindi hao kumi, wataingia katika mchuano wa fainali kutafuta tatu bora ambapo washindi watawajibika kuitetea miradi yao mbele ya jopo la majaji ili kupata miradi mitatu bora ambapo mshindi wa jumla atatangazwa na kupewa zawadi katika hafla maalum ya utoaji wa tuzo.
Sheria, taratibu, kanuni na vigezo vya shindano hili zinapatikana bure kwenye tovuti ya (http://startupper.total.com/) .
Shindano la « Startupper of the year by Total » ni juhudi za Kampuni ya kimataifa ya Total katika kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili kusaidia nchi zote duniani ambako kampuni ya Total ipo. Shindano hili ni hatua madhubuti yenye lengo la kuvumbua ubunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kuchangia uanzishwaji wa viwanda vidogo vitakavyotoa ajira na kuchangia maendeleo ya jamii na ya nchi za bara la Afrika kwa ujumla.
Shindano hili linalenga kuibua miradi mipya, iliyotokana na wananchi wenyewe ambayo inaendana na malengo ya jumla ya uwepo wa kampuni ya Total.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...