Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage imendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi utakaochezwa Novemba 07, mwaka huu jijini Dar es salaam katika uwanja wa Azam Chamazi.
Twiga Stars iliingia kambini Oktoba 29, katika hosteli za Shirikisho zilizopo Karume, ina kikosi cha wachezaji 22 wanaofanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa Karume.
Mchezo dhidi ya Malawi ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa, ambao kocha Kaijage atautumia kuangalia maendeleo ya wachezaji wake kwa ajili ya maandalizi ya micheo ya kimataifa.
Wachezaji waliopo kambini ni Asha Rashid, Estha Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Amina Ally, Fatuma Issa, Belina Julius, Happines Hezron na Donizia Daniel.
Wengine ni Maimuma Hamisi, Stumai Abdallah, Anna Hebron, Anastazia Anthony, Shelder Boniface, Wema Richard, Tumaini Michael, Jane Cloudy, Saada Ramadhani na Sofia Mwasikili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...