Kuimarika kwa uhifadhi wa misitu katika misitu ya tao la Mashariki iliyoko kwenye milima ya Usambara kumesaidia kuboresha shughuli za kijamii kwa wananchi wanaoishi kwenye vijiji kuzunguka misitu hiyo katika wilaya ya Muheza na Korogwe mkoani Tanga, mashamba haya ya mpunga ni katika kijiji cha Mkwakwani kata ya Mnyuzi wilaya ya Korogwe yamestawi vizuri kutokana na juhudi hizo za uhifadhi wa misitu, zinazofanywa na wadau mbalimbali wa uhifadhi ikiwemo wakala wa huduma za misitu nchini TFS na Mfuko wa kuhifadhi misitu ya tao la Mashariki EAMCEF juhudi ambazo zimesaidia kuimarisha mtiririko wa maji yanayotumika kwa shughuli za kijamii, ikiwemo kilimo cha umwagiliaji. Kilimo katika maeneo haya hakitumii mbolea wala kemikali za viwandani.
 Picha na Vedasto Msungu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...