UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umewaomba radhi wadau wa soka pamoja na shirikisho la soka nchini (TFF) kwa vurugu zilizotokea
kwenye mchezo wa baina yake na Mbeya City uliofanyika mwishoni mwa
wiki uwanja wa CCM Mkwakwani.
Mchezo huo wa ligi kuu Vodacom ulimalizika kwa vurugu hadi kikosi cha
kutuliza ghasia kilipoingilia kati na kutumia mabomu ya machozi
kuwatawanya mashabiki wa soka waliokuwepo katika uwanja wa Mkwakwani.
Vurugu hizo zilitokea kufuatia mwamuzi,Erick Enock kutoka Arusha
kuamuru ipigwe penati kuelekea lango la Coastala union katika dakika
za majeruhi na kuiwezesha Mbeya City kusawazisha bao hivyo hadi
matokeo kuwa sare ya fungana bao 1-1.
Coastal Union iliomba radhi katika barua yake iliyoandikwa na kutiwa
saini na Mwenyekiti wake,Dr Ahmed Twaha kwenda kwa Katibu mkuu wa TFF
na nakala kwa Rais Jamal Malinzi,afisa mtendaji mkuu bodi ya ligi na
katibu wa Chama cha soka mkoa wa Tanga (TRFA).
Aidha baada ya kutokea tukio hilo,Mwenyekiti huyo alisema alilazimika
kuitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji kujadili nini cha
kufanya na hatua za kuchukua kwa wale watakaobainika kuhusika kwenye
vurugu hizo.
Katika kikao hicho alisema kamati ya utendaji imelaani vurugu hizo na
imeaziamia kuwachukulia hatua waliohusika“Tunaomba radhi kwa TFF na
TRFA kwa matukio hayo yaliyofanywa oktoba
31,tunachukua ahadi klabu ya Coastal Union kufidia gharama za
uharibifu utakaothibitika na kuwachukulia hatu waliohusika”ilieleza
sehemu ya barua hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...