FREDDY MACHA: "Ulikuwa na wenzio Tanzania kwa miezi sita...kule Mbeya vijijini. Ulikuwa nna wananchi. Vipi ulijisikaje katika eneo hili la Afrika? "

EVELINA: "Lilikuwa jambo la kipekee. Ilitupa changamoto na utofauti mkubwa, ambao sintokwawia kurudia tena. Kama nilivyokueleza awali kila siku tuliyokuwa vijijini ilikuwa kama wadhifa fulani. Maana tulitaka ni kuwa sehemu mahsusi ya jumuiya...wenyeji walitukaribisha, walituhusisha katika mambo yao...tulikaa na familia zao, tunashukuru sana kwa hilo. Walifungua milango yao. Wakatukaribisha. 
Mara nyingi ilibidi kujifinya, na kujiuliza je kweli, Mungu wangu niko kweli Afrika? Na hisia hiyo ya kutoamini maastajabu haikunitoka kwa miezi yote sita niliyokuwa Tanzania! Ni uzoefu ulionibadili sana. Nadhani wanavijiji wengi walikuwa na wasiwasi kwamba sisi Wazungu tulikuwa wasafi au tungeshindwa kuishi yale maisha yao. Ilibidi wahimizwe kuwa hakuna noma yeyote..."

 Wanafunzi wanavijiji Lukata na Wageni waliowafundisha taaluma ya biashara. Picha ya Evelina Moceviciute

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...