Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja pamoja na Kamishna wa Nishati, Mhandisi Hosea Mbise hapo jana walifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali yanayopitiwa na mradi mkubwa wa Gesi Asilia.

Lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea shughuli zinazoendelea kwenye mradi wa gesi asilia pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa maeneo hayo kuhusu masuala mbalimbali ya shughuli zao za kila siku.

Maeneo ambayo yalitembelewa na viongozi hao ni pamoja na Kituo cha Kupokea Gesi Asilia ya Mtwara na Lindi cha Somangafungu (Somangafungu Gas Receiving Station) kilichopo wilayani Kilwa, mkoa wa Lindi; Visima vya gesi asilia vya Mnazi Bay na Msimbati; Sehemu iliyoathiriwa na Mmomonyoko wa ardhi ya Msimbati na Kituo cha Kuchakata gesi asilia cha Madimba cha mkoani Mtwara.

Wengine katika ziara hiyo ni Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Gesi Asilia, Mhandisi Norbert Kahyoza, Meneja wa Kampuni ya Gesi Asilia (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Ziara hiyo ni miongoni mwa mikakati iliyowekwa na viongozi hao kukagua shughuli mbalimbali za masuala ya Nishati na Madini kote nchini.
Baadhi ya mitambo katika Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia kutoka Songosongo na Mtwara kilichopo Somangafungu wilayani Kilwa Mkoani Lindi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (kulia) na Naibu wake, Mhandisi Paul Masanja (kushoto) wakimsikiliza Meneja wa Kampuni ya GASCO, Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) akiwaeleza kuhusu Kituo cha Kupokelea Gesi cha Somangafungu. Katikati ni Msimamizi wa Kituo hicho, Mhandisi Msafiri Peter.
Baadhi ya mitambo ya kupokelea gesi asilia iliyopo kwenye maeneo kilipo kisima cha gesi asilia cha Mnazi Bay Namba 3.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. HAYO MATUMBO YA HAO JAMAA WAWILI SIJUI NDIO MAWAZIRI KWA KWELI MUONEKANO WAO UNATISHA , HAPO INAONYESHA KANA KWAMBA WAO NJAA HAWAIJUI KABISA,HAPO KWELI KUNA KAZI TU?

    SIO KIOO KIZURI KWA JAMII, HATA KAMA SIO ULAJI LAKINI WAO NI KIOO CHA JAMII ATLEAST WAFANYE MAZOEZI YA KUPUNGUZA MATUMBO , HIO NOOOMA,

    WAIGE MFANO WA MAWAZIRI WENGINE DUNIANI KAMA ULAYA NA MAREKANI HAKUNA MTU MWENYE KITAMBI KAMA HIVYO, INATISHA ,. SASA WATANZANIA WAKIIGA HIO FASSION SI ITAKUWA TAABU KWELI HATA KAZI KWELI INAWEZA FANYJIKA KATIKA HALI HIYO?

    ANGALIENI AFYA ZENU NDIO MUHIMU KWANZA KABLA YA YOTE,..

    MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...