Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WANANCHI wa Kata ya Saranga Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kujitokeza kupiga kura ya Diwani Novemba 15 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty amesema kuwa kufanya uchaguzi huo kunatokana na kuharibika kwa uchaguzi wa Oktoba 25 ulisababishwa na vurugu.
Amesema wananchi wanaotakiwa kupiga kura kwa kata hiyo ni wale waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Natty amesema waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura ni 58,611 ambao ndio wataoruhusiwa kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa diwani wanayemtaka kuongoza kata hiyo.
Amesema vituo vya kupiga vitafunguliwa majira ya saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni na baada ya hapo zoezi likiwa limekamilika la uhesabiaji kura atatangazwa mshindi katika uchaguzi huo.
Uchaguzi wa diwani katika kata hiyo ilitokana na vurugu kubwa ambazo zilianza majira ya 11:000 asubuhi ilifanywa na baadhi ya wasimamizi wa vituo na watu wasiojulikana katika cha kugawa vifaa eneo TANROAD Temboni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...