BENKI  ya Barclays hapa nchini inatarajia kuwaletea wapenzi na Mashabiki wa soka kombe la ligi kuu ya Uingereza kwa ajili ya kupiga nalo picha ikiwa mwaka huu ni mwisho wa benki hiyo kudhamini ligi kuu nchini Uingereaza, Pia wananchi wameombwa kujitokeze kufungua akaunti kwa ajili ya mshara katika benki hiyo ili kujishindia tiketi mbili za kwenda kuangalia ligi kuu ya Uingereza.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar,Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera alifafanua kuwa  "Wapenzi wa soka wajitokeze kwa mujibu wa ratiba ya benki a Barclays kwaajili ya kugipatia picha wakiwa na kombe la benki hiyo ikiwa ni mwaka huu ni wa mwisho kudhamini ligi kuu ya Uingereza iliyokuwa ikijulikana kama Barclays Premier League." Bendera 

Nae Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa  amesema kuwa  Disemba 3 mwaka huu kombe hilo litaanzia katika tawi kuu la benki benki hiyo Posta kuelekea Mwembe yanga kupitia barabara ya Pungu mpaka Temeke Hospitali, Uwanja wa Taifa, kituo cha magari cha Mombasa na kumalizia viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Na Disemba 4 litaanzia kutembezwa kutokea katika benki ya Barclays tawi la Alpha kuelekea ofisi za IPP Media, Mlimani City, tawi la benki hiyo la Slip way Kinondoni Biafra, Mazese Darajani na kuishia katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam.

Aidha Mwakyusa aliyoa wito kwa wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupiga picha na kombe la ligi kuu ya Uingereza ambapo mwaka huu ni mwisho wa benki ya Barclays kudhamini ligi kuu Uingereza.
Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa na Kaimu mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera wakiwa wameshika picha ya kombe la mpira ambayo litatembezwa Disemba 3 na 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwaajili ya wapenzi wa mpira wa miguu kupiga nalo picha ikiwa mwaka huu benki ya Barclays ni mwisho wa kudhamini ligi kuu uingereza.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na benki hiyo kutembeza kombe la Barclays premier ligi ya Uingereza kulitemeza jijini Dar es Salaam kwaajili ya wapezi wa soka jijini hapa kupiga nalo picha ambazo itakuwa kumukumbu kwao.Kusoto ni Grace Josef na kulia ni Rhobina Justine wakiwa ni miongoni wa washiriki wa benki hiyo katika kutembeza kombe hilo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa akizungumza na waandishi wa habari kuhuriana na ratiba ya kombe hilo litakavyokuwa likizungushwa ili wapenzi wa soka kupiga picha na kombe ikiwa benki ya Barclays ni mwaka wa mwisho kudhamini ligi ya Uingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. The mdudu, tokeni kwenye usingizi mnene ndugu zangu watanzania amakweli usilolijua ni usiku wa giza na namuomba rais wetu Magufuli na serikali yake yote wapige stop ujinga ujinga kama huu swali dogo tu ningependa niwa ulizeni hivi hilo kombe la VPL la hapo Tanzania linaweza kuingia huku England? mimi nipo huku Uingereza so nawajua vizuri sana waingereza na tabia zao chafu 100% hilo kombe lingeishia uwanja wa Ndege na kuamliwa liludi huko Tanzania so kwa mtazamo wangu ndio maana soka la Tanzania yetu we have long way to get there haingii akilini kushabikia kitu cha mwezio kuliko chako hilo kombe la ligi ya England haliwezi kupelekwa nchi kama Brazil au Argentina wataanzia wapi na nani atawapokea coz ligi yao standard za mpira ni ovyo kabisa ila TV ndio zina kuongopeeni njoo huku uingie uwanjani kisha uone mauza uza yao kama utaenda siku nyingine kwa wachezaji hasa wa England wenyewe ndio bule kabisa ndio maana England yao kushinda kombe kubwa kama WORLD CUP kwao ni ndoto kitu ambacho nasema hakitokea so nakuombeni tupende vya kwetu kwanza vya wengine baadae so tusikate tamaa na matokeo ya Taifa Stars kufungwa 7 mbona Brazil kafungwa 7 na Germany lakini wamejipanga upya na wako on fire now so hata sisi Tanzania ni kujipanga vizuri tu tuna wachezaji wazuri sana tena tunao more talented than England players I love Taifa Stars na ntaendelea kuipenda daima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...