HALMASHAURI
ya Manispaa ya Kinondoni imeanzisha utaratibu kwa wananchi kutoa malalamiko juu
ya watoa huduma katika manispaa hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda amesema kuwa kuna watendaji wanashindwa kufanya kazi ambazo waliziomba
na kuifanya serikali ionekane ni kikwazo kwa wananchi wake.
Amesema
kuwa baadhi ya wafanyakazi wanachelewesha kutoa huduma ili kutengeneza
mfumo wa kupata rushwa na kusababisha shughuli nyingi za manispaa kushindwa
kusonga mbele kutokana na waomba rushwa kazini.
Makonda
amesema wananchi wanataka huduma kwa
wakati, kukosekana kwake kunafanya kuwepo kwa manung'uniko juu ya utendaji wa
waajiriwa kwa kuweka mazingira ya kufanya kazi kwa kutegemea rushwa .
“Hatuwezi
kuwa na wafanyakazi ambao kufanya kazi kwao mpaka wapate rushwa, wakati huku
wanapewa mshahara na mazingira mazuri kwa mujibu wa sheria ya wafanyakazi
katika serikali” amesema Makonda.
Aidha
amesema kuwa baada ya kupata malalamiko mengi dhidi ya idara au mtendaji hatua
za nidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria ikiwa ni kutaka watumishi wafanye
kazi bila kuweka mazingira yenye
rushwa.
Makonda
amesema kukiwa na malalamiko dhidi yake ya utendaji wake yatakweda kwa Mkuu wa Mkoa, hiyo yote ni kuonyesha kila mtu kuwajibika kutokana na wajibu na utaratibu
uliowekwa na serikali kwa watumishi wote.
Amesema
kuwa wananchi wanaweza kutuma katika hatua hizi Kinondoni ,Maelezo dhidi ya
huduma tatanishi, kwenda katika namba 15404 ambapo malalamiko yatapitiwa kila
wiki na kazi hiyo inafanywa na vijana watano wenye ujuzi na kutoa majibu bila
ya kumuonea mtu yeyote.
Makonda
amesema baada ya miezi mitatu mtumishi au mtendaji kwa kazi aliyofanya ikiwa ya
ufanisi atapata tuzo ikiwa ni kuonyesha kazi za serikali zinafanywa kwa mujibu
wa sharia na kufuata maadili yaliyowekwa kwa ajili ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...