Yoga & Karate Instructor.
Mazoezi ya Yoga, hayawezi lingalishwa na aina nyinginezo za mazoezi ya
nguvu za misuli. Mbinu za kiundani zenye maigizo ya mikao ya wanyama tofauti,
na kupitia mtililiko wa kuvuta pumzi, una imarisha sana nguvu mwilini
kuringanisha na mazoezi ya aina yeyote ya nguvu na misuli ambayo mwisho wa
zoezi mwili unakuwa umechoka, wakati yale ya Yoga, mwili unakuwa umejenga nguvu
zaidi.
Kuna
dalli nyingi za kupungukiwa na
usawa wa kemikali ijulikanayo kama “Hormones” ndani ya damu mwilini mwa mtu. Baadhi ya mapungufu ambayo
hubainika mapema ni pamoja na:
ü Kuumwa kichwa
ü Matatizo ya
ngozi, kuwashwa au kuwa na mapele madogo.
ü Maumivu ya
viungo
ü Hali ya kutoweza
pata usingizi.
ü Uchovu
ü Kupungua kwa
hamu ya unyumba au ngono.
ü Wepesi wa kuwa
na hasira
ü Ongezeko la
uzito mwilini.
ü Kuzeeka haraka.
Mazoezi ya Yoga ya nauwezo wa kuzisisimua sehemu
hizo za “Glands” na kuziamsha kwa kuweza kufanya kazi yake ya kusawazisha na
kumiliki usawa wa“Hormones” mwilini.
Mfumo
mzima wa “ Endocrine” ni kama ufuatavyo:
The
Glands ni sehemu ya
mwili kama kifuko mnamo fanyizwa maji
yenye dawa yaingiayo damu au damuni na kufanya kazi nyinginezo mwilini kwa mizani na
makadilio sahihi. Endapo kazi yake itakuwa imevuka au kushuka, pia huleta
madhara mwilini na matokea yake ni kuwa na baadhi ya hizo tabia zilizoelezwa
hapo juu awali. Kemikali inayo chakachuliwa na hizo Glands, inajulikana kama
“Hormones”. Hizi “Hormones” zina ushawishi mkubwa katika maisha ya mwanaadam,
ikiwemo; makuzi ya mwili, kusaga na kuyeyusha chakula, nguvu za mwili, isitoshe
na joto la mwili, ngono, kuhifadhi au
kuweka maji mwilini. Hivyo, zifuatazo
hapa ni kazi na majukumu ya kila moja ya “Gland” na madhara yake isipofanya
kazi inavyostahili.
Hii imekaa ipo katikati ya ubongo wa mwanaadam. Inakiwango kikubwa cha kupokea damu Zaidi ya
viungo vingine vyote vya “Glandular” mwilini. Kazi kubwa ya Pinea Gland ni kuchakachua hormone itwayo “Melatonin” ambayo
inawajibika kuhakikisha maendeleo ya hali ya kuwa “kiume” au “kike”
mwilini mwa binaadam; “Seratonin”,
ambayo ni “Hormone” muhimu kwa maendeleo ya akili pia.
Pia, hii “Gland”, inakazi nyingine ambayo ni kuangalia madadiliko ya tabia ya mwili za kila siku kama vile mabadiliko ya jinsi unavyo lala usiku au pengine
mchana.
2. Pituitary
Gland: Hii imepewa jina na tasisi za sayansi ya madawa kama” Master Gland”, katika ukweli wa kazi yake hii nikama mnara wa usambazao
mawasiliano kwenye ubongo, sehemu ijulikanayo kama” Hypothalamus” ni kiungo
ndani ya ubongo kinacho miliki
mawasiliano ya mishipa ya fahamu kati ya mfumo wa “Glandular “na jinsi
mwili unavyo kuwa katika hali ya huzuni, sikitiko au furaha. Hii “Gland” pia
humiliki hali ya makuzi na kurekebisha joto mwili. Pungufu la au ongezeko la
kazi yake, husababisha makuzi yasio kawaida na kuwa kibonge au mbilikimo.
3.
Thyroid & Parathyroid Gland: imekaa shingoni, na inamiliki mabadiliko ya
chakula kilicho liwa mwilini
“Metabolism”, na kumiliki kima cha joto mwilini”Body heat”. Hali
kadhalika makuzi na uchafu ndani ya mwili. Panapokuwa na kasoro ya udogo au
ukubwa wa miliki hii, matokeo yake ni kukasirisha mishipa ya fahamu mwilini na
kuwa hoi au kuchoka kila mara. Calcium na phosphorus zinamilikiwa na hii Gland.
4. Thymus
Gland: Ipo katika
ya kifua, na huwa kubwa mno utotoni na mtoto afikiapo barehe inapungua kuwa
robo ya umbo lake. Hii ni silaha ya kinga za mwili kwa mashambulizi ya magonjwa
ya nje ndani ya mwili. Ina miliki
udumishaji ulinzi wa kupambana na magonjwa nayayo shambulia mwili.
5. Adrenal
Glands:
Hii ipo juu kidogo ya mafigo, kazi yake hasa ni kutoa nguvu na moto la
hali ya juu na kuamua penye jambo la hatari au tukio, hisia ya mwanaadam aidha uamua kukimbia au
kupigana kijasili kwa kupambana na tukio lolote.
6. Pancreas:
ipo chini kidogo ya tumbo na kazi yake ni kuyeyusha kemikali ijulikanoyo kama
“Enzyme”. Katika utumbo mdogo, inachanganya “Insulin” hormone inayo punguza
nguvu za sukari katika damu. Endapo
Pancreas inashindwa kumiliki vyema utengenezaji wa
Insulin mwilini, basi sukari ya damu huimalika Zaidi katika mwili na matokeo
yake ni Diabetes mellitus au ugonjwa wa kisukari. Pia papo hapo, Insulin
nyingi nayo sio nzuri, husababisha kutetemeka na udhaifu mwilini.
7.
Gonards:
Uume au uuke, na kazi yake ni kumiliki kazi ya ngono. Zina changanya Endrogen
ambayo ni hormone ya jinsia ya kiume, pia Estrogen kwa wanawake. Hizi zote zinafanya kazi ya
tabia ya mwili wa kike na kiume kwa jinsia zilivyo tofautiana.
Maumbile ya mwili mzima wa mwanaadam , inamilikiwa
na hizo Hormones. Hapo ndipo utakuta, kupitia mazoezi ya aina ya
“ Yoga Asanas”, mwili unaweza
kumiliki na kusawazisha mzani wenye kima cha wastani katika uchanganyaji wa hizo hormones mwilini.
Mafunzo ya
mazoezi ya Yoga, yanadhihirisha wazi kutokana na masomo mbalimbali ya uchunguzi
toka vyuo vikuu vingi maarufu nchini
Marekani na kuandikwa kwa majarida mbali mbali yenye malengo ya kuielimisha
jamii kuhusu afya na maumbile kupitia mazoezi ya Yogasanas.
Imeandikwa na mwalimu wa Yoga, Rumadha Fundi kupitia
majarida ya chuo alicho somea filosofia
ya Yoga cha “College of Neo Humanist
Studies”, Gullringen, Sweden na pia Tiljala, Culcutta, West Bengal, India ’87.
Wewe Chezea Sensei Rumadha Fundi huyu ni Profesa ktk hii kitu Yoga na pia sanaa ya Karate. mwendo huo huo sensei !
ReplyDeletewadau FFU-ughaibuni
Freddy Macha somo hilo umelisoma? wewe karaga bao mjini shule kijijini jembe
ReplyDelete