JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
Anuani ya Simu “TAMISEMI” DODOMA
Simu Na: (026) 2322848, 2321607,
2322853, 2322420,
Nukushi: (026) 2322116, 2322146.
2321013,
Barua pepe:ps@poralg.go.tz
|
|
Tawala
za Mikoa
na
Serikali za Mitaa,
S. L. P.
1923, DODOMA.
|
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi
wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa
Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na
Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015
kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.
Kutokana
na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa
Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu
wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.
Agizo
hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea
malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa
mazingira ya rushwa.
Katika
uchunguzi ambao umefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
imegundulika kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa
hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha
shilingi Milioni 75.
Aidha,
Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote
nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji
apate leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.
Mhe.
Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika
kutoa leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Imetolewa na:
Rebecca
Kwandu
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi
ya Rais - TAMISEMI
30
Desemba, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...