Kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma za kibunifu imetunikiwa tuzo
mbili za ubora za Tanzania Leadership Awards 2015 katika halfa
iliyofanyika katika hotel ya Hyatt jijini Dar es salaam.
Airtel imejishindia tuzo hizo katika kipengele cha matumizi bora ya
huduma za kimtandao kufikia wateja wake (best use of social Media in
marketing) pamoja na kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja
(brand excellence) katika sekta ya mawasiliano na kuwashinda makapuni
mengine yaliyokuwa wakichauana nayo katika kinyanganyiro cha tuzo hizo
Wakionge wakati wa kukabidhi tuzo hizo , waandaaji wa tuzo hizo za
Tanzania Leadership Awards, Kishore Bollakpalli alisema " Airtel
imepata tuzo hizi kutokana na kufanya vizuri zaidi katika kuwasiliana
na wateja wake kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na hivyo
kuwafikia wateja wake nchini nzima kwa urahisi zaidi.
Lakini kwa
upande wa tuzo ya Brand excellence, Airtel imeonyesha kwa vitendo
dhamira yao ya kutoa huduma bora kwa wateja wake huku ikitoa bidhaa na
huduma za kibunifu ili kukidhi mahitaji ya wateja wake na kuboresha
maisha yao.
Akipokea tuzo hizo Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso
alisema" Tunayofuraha kupokea tuzo hizi za Tanzania Leadership award
na tunaamini huu ni ushuhuda kamili unaoonyesha kwa vitendo dhamira
yetu ya kutoa huduma zenye zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu
zikiwemo huduma za intaneti, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi
na kuchochea kukua na upatikanaji wa huduma za kifedha nchini".
Colaso aliongeza kwa kusema Airtel itaendelea na dhamira yake yakutoa
huduma zinazogusa mahitaji ya wateja wake u na kuwaweka karibu ili
kuendelea kutoa huduma bora zaidi katika miaka ijayo.
Tuzo za Tanzania Leadership Awards zinalenga kutambua na kupongeza
jitihada zinazofanya na watu binafsi na makapuni katika kuboresha
uchumi wa Tanzania na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso akipokea tuzo ya ubora
katika kipengele cha kutoa huduma za kimtandao kutoka kwa waandaaji
wa tuzo za Tanzania Leadership Award, Kishore Bollakpalli
(kushoto). Airtel Tanzania imejishindia tuzo mbili za ubora katika
kipengele cha kutoa huuduma za kimtandao pamoja na huduma zinazokidhi
mahitaji ya wateja.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso akionyesha tuzo mbili za
ubora mara baada ya kukabidhiwa na waandaji wa Tanzania Leadership
Award 2015. Airtel ilijishindia tuzo hizo katika kipengele cha kutoa
huuduma za kimtandao pamoja na huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja
katika sekta ya mawasiliano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...